KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, August 15, 2011

Los Angeles Galaxy KUFANYA USAJILI WA KEAN HII LEO.

Mshambulaji kutoka jamuhuri ya Ireland pamoja na Tottenham Hotspurs Robbie Keane bado anasubiri hatua za kukamilishwa kwa usajili wake wa kujiunga na klabu ya Los Angeles Galaxy ya nchini Marekani.

Robbie Keane anasubiri kukamilishwa kwa hatua hiyo huku uongozi wa LA Galax ukiwa tayari kutoa kiasi cha paund million 3.5 kama ada ya uhamisho wake.

Kusubiri kwa mshambuliaji huyo kunatokana na usajili wa nchini Marekani kutarajia kukamilishwa hii leo, huku kila upande ukiamini kila kitu kitakwenda sawa kabla ya saa kumi na moja alfajiri kwa saa za nchini Uingereza ambapo ukanda wa Marekani itakua saa sita usiku.

Msemaji wa Los Angeles Galaxy amesema wanaamini watampata Robbie Keane kufautia kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha Spurs, hatua mbayo ilipelekea kupelekwa kwa mkopo kwenye klabu ya West Ham Utd ambayo ilishuka daraja msimu uliopita.

Mpaka sasa Los Angeles Galaxy, wameshafanya usajili wa wachezaji waliowahi kutamba na wanaotamba ulimwenguni kama David Beckham, Landon Donovan pamoja na Juan Pablo Angel huku wakiamini ujio wa Kean utaendeleza chachu ya mvuto wa kikosi chao.

No comments:

Post a Comment