KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 25, 2011

JAMANI HAYA NI MAISHA YANATAFUTWA KILA SEHEMU - SAMIR NASRI.


Baada ya kukamilisha usajili wa kujiunga na Man City jana jioni, kiungo kutoka nchini Ufaransa Samir Nasri amesema hana cha kupoteza zaidi ya kuanza mipango ya kuitetea klabu hiyo yenye maskani yake Etihad Stadium.

Samir Nasri ametangaza mpango huo akiwa mjini Manchester ambapo amesema amefurahishwa na hatuaya kukaribishwa vyema na mashabiki wa Man City ambao walionekana kumlaki kwa shangwe tena kwa kutaka wapige nae picha pamoja na kusaini sehemu ya jezi na vitabu vyao vya kumbukumbu.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24, pia amegusia hatua ya kuondoka kwake Arsenal ambapoa mesema kila mmoja anatakiwa kutambua hiyo ni sehemu ya maisha yake ambayo kila siku imekua ikihitaji changamoto mpya.

Katika hatua nyingine Samir Nasri amemshukuru kila mmoja anaehusika na Arsenal kwa kusema waliishi vizuri katika kipindi cha misimu mitatu aliyokuwepo huko Emirates na pia akatoa salamu za kila la kheri.

Samir Nasri amekamilisha uhamisho wake kutoka Arsenal kuelekea Man City kwa gharama ya paund million 24, baada ya kugoma kusaini mkataba mpya na The gunners ili hali mkataba wake uliokua unaendelea ulitarajia kufikia kikomo mwishoni mwa msimu huu.

No comments:

Post a Comment