KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, August 22, 2011

Juan Mata KUICHEZEA CHELSEA.


Uongozi wa klabu ya Valencia umethibitisha kufikia makubaliano ya kuuzwa kwa kiungo kutoka nchini humo Juan Mata baada ya kufanya mazungumzo na viongozi wa klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza.

Valencia wametangaza kufikia hatua hiyo huku uongozi wa Chelsea ukikubali kutoa kisi cha paund million 23.5 ambazo ni sawa na euro million 27, kama ada ya uhamisho wa kiungo huyo ambae pia aliwahi kuhusishwa na taarifa za kutaka kusajiliwa na Arsenal.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23, hii leo alitarajiwa kuelekea jijini London kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya ikiwa ni sehemu ya kukamilisha mipango ya usajili wake ambao utamfanya kuwa mchezaji wa nne kuelekea Stamford Bridge mara baada ya kuwasili kwa meneja mpya kutoka nchini Ureno Andre Villas Boas.

Wachezaji wengine ambao tayari wameashasajiliwa huko Stamford Bridge chini ya Andre Villas Boas ni Oriol Romeu akitokea Barcelona ya Hispania, Romelu Lukaku akitokea Anderlecht pamoja na kipa Thibaut Courtois akitokea Genk FC.

Katika kipindi cha misimu mitatu Valencia wamekubali kuwatoa wachezaji wao watatu ambao ni nyota ambapo kwa mara ya kwanza walikubali kumuachia mshambuliaji David Villa ambae alisajiliwa na Fc Barcelona kisha wakakubali kumuuza David Silva katika klabu ya Manchester City na sasa wamekubalia kumuuza Juan Mata.

Andre Villas Boas mwishoni mwa juma lililopita alimzungumzia Juan Mata katika mkutano na waandishi wa habari ambapo alisema mchezaji huyo sifa zake zinajieleza na ndio maana walikua wakimuwania.

No comments:

Post a Comment