KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, August 12, 2011

Manuel Jose KATIKA MTIHANI MKUBWA USIKU HUU.


Meneja wa klabu ya Al Ahly ya nchini Misri Manuel Jose amesema kikosi chake usiku huu kitakua na kazi ya ziada ya kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika mchezo wa mzunguuko wa tatu wa ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Mouloudia Alger ya nchini Algeria.

Manuel Jose amesema mchezo huo utakaochezwa mjini Cairo, utakua na upinzani mkali kufautia uwezo wa wapinzani wao ambao mpaka sasa wanamiliki point moja katika msimamo wa kundi la pili sawa na kiksoi chake ambacho pia kina point moja.

Amesema wanachotakiwa kufanya ni kupata ushindi ili kuweza kujitengenezea njia ya kusonga mbele katika michuano hiyo mikubwa barani Afrika na endapo watashindwa kufanya hivyo hali yao itaendelea kuwa tete na pengine watafifisha matumaini waliyojiwekea.

Katika hatua nyingine meneja huyo kutoka nchini Ureno ametetea kikosi chake ambacho kwa sasa kina damu changa, kwa kusema kina uwezo wa kushindana huku akiwashangaa wanaokibeza kikosi hicho kwa kusema hakina uwezo wa kuhimili mikiki mikiki ya michuano ya kimataifa.

Klabu ya Al-Ahly ambayo tayari imeshatwaa taji la barani Afrika mara sita ilianza kulaumiwa na baadhi ya mashabiki huko nchini Misri, baada ya kuondoka kwa kipa Essam Al Hadary, beki Wael Gomaa pamoja na Mohamed Aboutrika.

Al Hadary kwa sasa anaitumikia klabu ya El-merekh ya nchini Sudan.

No comments:

Post a Comment