KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, August 13, 2011

Peter Osaze Odemwingie KUBAKI PALE PALE.


Ndoto za mshambuliaji kutoka nchini Nigeria Peter Osaze Odemwingie za kutaka kuihama West Bromich Albion zimeingia dosari baada ya uongozi wa klabu hiyo kuikataa ofa ya klabu ya Wigan Athletic iliyopania kufanya hivyo kabla ya August 31.

West Bromich Albion wameikataa ofa ya Wigan Athelecs huku wakieleza wazi kwamba hawapo tayarui kumruhusu mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30 kuondoka katika kipindi hiki kufuatia mipango iliyowekwa huko The Heathens.

Mkurugenzi wa michezo wa West Bromwich Albion Dan Ashworth amesema hakuna wanachokificha juu ya msimamo wao na ndio maana wamewaeleza wazi Wigan suala la kutokua tayari kuuzwa kwa Peter Osaze Odemwingie ambae msimu uliopoita alifanikiwa kupachika mabao 15.

Amesema kwa sasa wanafanya mazungumzo na mshambuliaji huyo juu ya kusaini mkataba mpya na wanaamini kila kitu kitakwenda vizuri, hivyo litakua jambo la kipuuzi endapo watabadilisha muelekeo wa mipango waliyoiweka.

Peter Osaze Odemwingie alijiunga na West Brom mwezi August mwaka 2010, akitokea nchini Urusi katika klabu ya Lokomotiv Moscow kwa ada ya uhamisho wa paund million 1.5.

No comments:

Post a Comment