KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 23, 2011

Radamel Falcao ATAMBULISHWA KWA MASHABIKI VICENTE CALDERON.

Uongozi wa klabu ya Atletico Madrid, hii leo umemtambulisha rasmi mshambuliaji kutoka nchini Colombia Radamel Falcao, baada ya kukamilisha taratibu za uhamisho wake ulioigharimu klabu hiyo Euro million 40 akitokeea FC Porto.

Utambuklisho huo uliofanyika katika uwanja wa Vicente Calderon uliopo mjini Madrid, ulishuhudia mashabiki 15,000 wakijitokeza kumlaki huku wakionyesha furaha ya kusajiliwa kwa mshambulioaji huyo ambae msimu uliopita aling’ara kufuatia kupachika mabao 38.

Radamel Falcao, alijitokeza mbele ya mashabiki hao huku akiwa amevalia jezi ya Atletico Madrid yenye nambari tisa mgongoni ambapo kitendo hicho kiliendelea kuwapagawisha mashabiki hao ambao siku za hivi karibuni walionyesha kuhuzunishwa na kitendo cha kuondoka kwa mshambuliaji kutoka nchini Argentina Sergio Ag├╝ero alietimkia Man City.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alipata nafasi ya kuzungumza na mashabiki ambapo amesema ni furaha sana kwake kujiunga na klabu ya Atleticio Madrid ambayo sasa inampa nafasi ya kumbadilishia mazingira ya soka lake.

Amesema kwa ufahamu huo atahakikisha anaendeleza uwezo wake na kuisaidia Atletico Madrid kufikia malengo na ikiwezekana kutwaa mataji makubwa nchini Hispania na barani Ulaya kwa ujumla.

Kusajiliwa kwa mshambuliaji huyo huko Vuicente Calderon huenda kukatoa mwanya kwa mashambuliaji mwingine wa Atletico Madid Diego Forlan kuondoka ambapo tayari ameshaanza kuhusishwa na taarifa za kutakiwa na mabingwa wa soka duniani upande wa vilabu Inter Milan.

No comments:

Post a Comment