KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, August 19, 2011

Radamel Falcao KUIHAMA FC PORTO.


Atletico Madrid wamekubalia dili la kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Colombia Radamel Falcao akitokea kwa mabingwa wa ligi ya barani Ulaya msimu wa mwaka 2010-11 FC Porto.

Ateltico Madrid wamekubali dili hiLo kwa kutoa kiasi cha Euro million 40, ambazo zitawasilishwa Estádio do Dragão, endapo Radamel Falcao atakamilisha vyema zoezi la kupimwa afya yake.

Mazungumzo ya kusajiliwa kwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25, hapo awali yaliwafanya viongozi wa Atletico Madrid, kuomba wapunguziwe ada ya uhamisho ambapo walitakiwa kutoa kiasi cha Euro million 47, ambacho kilipunguzwa na kufikia million 40.

Radamel Falcao anaondoka Estádio do Dragão, akiacha historia itakayokumbukwa daima ya kupachikma mabAo 38 msimu uliopita ambayo yalichangia kwa kiasi kikubwa kuiwezesha Fc Porto kutwaa ubingwa wa nchini Ureno pamoja na kutwaa ubingwa ligi ya barani Ulaya kwa kuichapa Fc Braga huko Dublin arena jamuhuri ya Ireland.

Miongoni mwa mabao hayo 38, yalimfanya mshambuliaji huyo kuibuka kidedea katika nafasi ya ufungaji bora kwenye michuano ya barani Ulaya ambayo ilifikia tamati huku akiwa amepachika mabao 17.

Kwa ujumla Radamel Falcao ameitumikiwa Fc Porto katika michezo 84 na kupachika mabao 73, baada ya kusajiliwa mwezi July mwaka 2009 akitokea nchini Argentina alipokua akiitumikia River Plate kwa ada ya uhamisho wa Euro million 5.5.

Sababu kubwa ya kusajili kwa mshambuliaji huyo kutoka nchini Colombia, imetokana na kuondoka kwa Sergio Aguero huko Estadio Vicente Calderon na kuelekea Etihad Stadium yalipo makao makuu ya klabu ya Manchester City ambayo ilikubali kutoka paund million 38 kama ada ya uhamisho wake.

No comments:

Post a Comment