KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 2, 2011

Raul Gonzales Blanco KUBAKI UJERUMANI.

Bossi wa klabu ya Schalke 04 Ralf Rangnick amekanusha vikali mipango ya kutaka kuuzwa kwa mshambuliaji kutoka nchini Hispania Raul Gonzales Blanco ambae yasemekana huenda akarejea nyumbani kwao kujiunga na klabu iliyopania kufanya mapinduzi katika ligi ya La Liga msimu ujao FC Malaga.

Ralf Rangnick amekanusha taarifa hizo kwa msisitizo mkubwa, ambapo ameeleza wazi kwamba taarifa za mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 34 kutakiwa nyumbani kwao si za kweli na bado wataendelea kuwanae klabuni hapo kama mkataba wake unavyoelekeza.

Amesema kila kukicha pamekua na taarifa tofauti juu ya Raul Gonzales Blanco, lakini ukweli ni kwamba amewathibitishia kupendezwa na mazingira ya Veltins-Arena, ambapo amaeahidi kujituma zaidi ya msimu uluiopita kwa ajili ya kuleta mafanikio zaidi.

Hata hivyo Ralf Rangnick, ametanabai kwamba ikitokea FC Malaga wakituma ofa ya kutaka kumsajili Raul, bado hawatokua tayari kumuachia, kutokana na kuamini kwamba uwepo wake huko nchini Ujerumani unatoa changamoto kwa vijana wengine chipukizi wa Schalke 04 kujifunza kupitia kwake.

kama itakumbukwa vyema, Raul Gonzales Blanco tayari alishawahi kuikataa mipango ya kuondoka Veltins Arena, kufuatia zogo la kusajiliwa kwake kutawala miezi miwili iliyopita ambapo kwa kipindi hicho alilengwa kusajiliwa na klabu ya Besiktas ya nchini Uturuki.

No comments:

Post a Comment