KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, August 13, 2011

Robbie Keane KUTIMKIA MAREKANI.


Uongozi wa klabu ya Los Angeles Galaxy umethibitsiha taarifa za kutaka kumsajili mshambuliaji kutoka Jamuhuri ya Ireland pamoja na klabu ya tottenham Hotspurs ya nchini Uingereza Robbie Keane.

Uongozi wa klabu ya Los Angeles Galaxy umesema mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31, huenda akajiunga na klabu hiyo wakati wowote kuanzia juma lijalo na kama itashindikana, basi watajitahidi kabla ya August 31 ambapo itakua mwisho wa harakati wa usajili huko barani Ulaya.

Uongozi huo umesema kusajili kwa mshambuliaji Robbie Keane kutaleta changamoto kubwa katika kikosi cha LA Galax, ambacho kwa miaka kadhaa sasa kimekua kikichagizwa na uwepo kwa kiungo hodari kutoka nchini Uingereza David Beckham aliesajiliwa akitokea Real Madrid ya nchini Hispania .

Robbie Keane msimu uliopita alipelekwa kwa mkopo West Ham Utd baada ya kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Spurs, na kwa bahati mbaya alishindwa kuonyesha uwezo wake huko Upton Park na kujikuta akizama na The Hammers walioshuka daraja.

Hata hivyo mshambuliaji huyo tayari alishawahi kuuzwa na uongozi wa Tottenham Hotspurs mwaka 2008 ambapo alisajiliwa na Liverpool na kisha alirejeshwa White Hert Lane baada ya kuingizwa katika mapendekezo ya meneja Harry Redknnap.

Robbie Keane, pia alishawahi kuvitumikia vilabu kama Wolverhampton Wanderers , Coventry City, Internazionale pamoja na Leeds United.

No comments:

Post a Comment