KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 16, 2011

Roberto Mancini AMTABIRIA MAKUBWA Sergio Aguero.Baada ya ushindi wa mabao manne kwa sifuri uliopatikana jana kwenye uwanja wa Etihad dhidi ya klabu iliyopanda daraja Swansea FC, meneja wa Man City Roberto Mancini amemtabiriwa mema mshambuliaji mpya wa kikosi chake Sergio Aguero.

Mancini amemtabiri mema mshambuliaji huyo alimsajili akiotokea Atletico Madrid, kufautia uwezo aliouonyesha jana, na kupelekea kufunga mabao mawili kati ya manne yaliyowapa ushindi Man city wakiwa nyumbani.

Mancini amesema mshambuliaji huyo bado yupo fit na ana uwezo wa kuonyesha uwezo mkubwa zaidi ya ule alioudhihirisha machoni mwa mashabiki wa soka ulimwenguni usiku wa kuamkia hii leo hivyo kwa upande wake hana shaka na hilo.

Amesema anatambua amemsajili mchezaji wa aina gani, na ndio maana anayazungumza hayo kwa kujiamini huku akimtakia kila la kheri Sergio Aguero mwenye umri wa miaka 23.

Sergio Aguero, amesajiliwa na Man City katika kipindi hiki akitokea Atletico Madrid kwa ada ya uhamisho wa paund million 38, huku lengo kubwa likiwa ni kuziba nafasi ya Carlos Tevez alieibua songombingo la kutaka kuondoka Etihad Stadium.

Mabao mengine ya Man City katika mchezo huo yalipachikwa wavuni na mshambuliaji kutoka nchini Bosnia Edin Dzeko, pamoja na kiungo kutoka nchini Hispania David Silva.

No comments:

Post a Comment