KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, August 5, 2011

SPURS WAANGUKIA KWA MAJIRANI.

Nayo klabu ya Tottenham Hotspur imepangwa kuanza na Hearts katika mchezo wa hatua ya mtoano ya ligi ya barani Ulaya *Europa Legue*.

Spurs ambao walifanikiwa kufika katika hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya msimu uliopita, msimu huu wameangukia katika michuano ya ligi ya barani Ulaya kufuatia kushindwa kumaliza katika nafasi nne za juu kwenye msimamo wa ligi ya nchini Uingereza msimu uliopita.

Hata hivyo bado inaaminiwa kikosi cha klabu hiyo ya jijini London kina uwezo mkubwa wa kufaulu mtihani wa mchezo huo wa hatua ya mtoano kufuatia uzoefu uliopatikana msimu uliopita katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Klabu nyingine ya nchini Uingereza iliyoingia katika ratiba ya hatua ya mtoano ya ligi ya barani ni Fulham ambayo imefanikiwa kufikia hapo baada ya kuitupa nje ya michuano hiyo klabu ya RNK Split ya nchini Croatia, na sasa watakutana na klabu ya Dnipro ya nchini Ukraine.

Mabingwa wa kombe la ligi nchini Uingereza *Carling Cup* Birmingham City watakutana na klabu ya nchini Ureno Nacional, huku Stoke City waliomaliza katika nafasi ya pili kwenye michuano ya kombe la FA wakiangukia kwa FC Thun ya nchini Uswiz.

Michezo hiyo ya hatua ya mtoano ya ligi ya barani Ulaya itachezwa August 18 na michezo ya marudio itapigwa August 25.

No comments:

Post a Comment