KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, August 29, 2011

Yossi Benayoun AJIWEKA NJIA PANDA MWENYEWE.


Kiungo kutoka nchini Israel Yossi Benayoun amepasua ukweli wa kufikiria safari ya kuikacha klabu ya Chelsea kufuatia mazingira ya klabu hiyo kuendelea kumbana siku hadi siku.

Yossi Benayoun amepasua ukweli huo kupitia ukurasa wake wa mtanyao wa Twiter ambao umesomeka “nipo njiani kuondoka Stamford Bridge”.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31, amelazimika kueleza ukweli kutokana na uhalisia wa kikosi cha Chelsea hivi sasa ambacho huenda kikamtumia sana kiungo kutoka nchini Hispania Juan Mata aliesajiliwa juma lililopita akitokea Valencia.

Mbali na mpango huo pia Yossi Benayoun, huenda akaendelea kukabiliwa na upinzani mzito endapo Chelsea watakamilisha usajili wa kiungo kutoka nchini Croatia pamoja na klabu ya Tottenham Hotspurs Luka Modric.

Mpaka sasa Yossi Benayoun ameshaitumia Chelsea kwa dakika moja toka msimu huu ulipoanza, hali ambayo inaendelea kumtia simanzi na kujihisi hahitajiki tena chini ya utawala wa meneja mpya kutoka nchini Ureno Andre Villas Boas.

Taarifa zilizopo zinadai kwamba Newcastle Utd wanajiandaa kumsajili kiungo huyo kwa ada ambayo mpaka sasa haijawekwa wazi.

Msimu uliopita Yossi Benayoun aliitumikia Chelsea katika michezo 10 na baada ya hapo alikubwa na majeraha ya kisigino ambayo yalimuweka nje ya uwanja kwa kipindi kikefu kabla ya kurejea tena uwanjani mwishoni mwa msimu.

No comments:

Post a Comment