KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, August 10, 2011

ZOGO LAZUSHA HOFU NSDANI YA CHAMA CHA SOKA UINGEREZA.

Zogo linaloendelea jijini London pamoja na baadhi ya miji ya nchini Uingereza, huenda likahatarisha kuanza kwa ligi kuu ya soka nchini humo iliyopangwa kuanza mwishoni mwa juma hili katika viwanja kumi tofauti.

Zogo hilo ambalo hii leo limeingia katika siku ya tano, limezusha hofu hiyo kufuatia sababu za kiusalama ambazo zimatazama sana upande wa mashabiki ambao wanatajia kuzishangilia timu zao zitakapoanza harakati za kuwania ubingwa wa msimu wa mwaka 2011-12.

Taarifa zilizopatikana mapama hii leo limeeleza kwamba, endapo zogo hilo halitomalizwa kwa wakati kutakuwa na uwezekano mkubwa wa michezo hiyo kutokuwepo kwa ajili ya kutoa nafasi kwa jeshi la polisi kufanya kazi yake ya kuzima matatizo yanayoendelezwa katika mitaa mbali mbali ya miji iliyokumbwa na kadhia hiyo.

Hapo awali taarifa zilieleza kuwa, michezo ambayo itachezwa katika jiji la London mwishoni mwa juma hili kati ya Tottenham v Everton, Fulham v Aston Villa pamoja na QPR v Bolton ilikuwa katika mashaka makubwa, lakini saa kadhaa baadae iliijumuisha michezo mingine itakayochezwa nje ya jiji hilo.

Hata hivyo uongozi wa chama cha soka nchini Uingereza FA kinasubiri kauli itakayotolewa na jeshi la polisi ndani ya saa 48 zijazo, ambayo itaidhinisha ni michezo ya mji gani itastahili kuanza na ipi italazimika kusubiri hadi hapo hali itakapokua shwari.

Zogo hilo lililoanza usiku wa kuamkia siku ya jumapili mwishoni mwa juma lililopita limesababisha mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya Uingereza dhidi ya Uholanzi uliokua umepangwa kufanyika hii leo katika mji wa London kuahirishwa na chama cha soka FA.

Pia mchezo mwingine uliotakiwa kuchezwa jana jijini London katika uwanja wa Vicarage Road kati ya Nigeria dhidi ya Ghana nao uliahirishwa kufuatai sababu za kuhofia usalama wa mashabiki walipanga kuhudhuria kweye mchezo huo.

No comments:

Post a Comment