KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, September 28, 2011

Sir Alex Ferguson AWAITA WACHEZAJI WAKE WAZEMBE.

Uzembe na kutokua makini ni maneno yaliyokua yametawala katika mazungumzo ya meneja wa Man utd Sir Alex Ferguson dhidi ya waandishi wa habari mara baada ya mchezo wa jana wa kundi la tatu ambapo mashetani wekundu walilazimisha sare dhidi ya mabingwa wa soka toka nchini Uswiz Fc Basle.

Sir Alex Ferguson alitumia maneno hayo kwa kuwalaumu wachezaji wake ambao walionyesha uwezo mkubwa katika kipindi cha kwanza ambacho kilishuhudia wakielekea mapumziko huku wakiongoza mabao mawili kwa sifuri lakini hali iliwabadilikia katika kipindi cha pili.

Amesema endapo wachezaji wake wangekuwa makini na kulinda mabao mawili yaliyopatikana katika kipindi cha kwanza kulikua na ulazima wa kuongeza bao lingine na pengine kupata point tatu muhimu ambazo zingewapa nafasi ya kukaa pazuri katika msimamo wa kundi la tatu.

Nae meneja wa Fc Basle Thorsten Fink amepasua ukweli wa kile kilichopelekea wachezaji wake kuonyesha juhudi na kufanikia kurejea katika mchezo na mwishowe kulazimishwa sare ya mabao matatu kwa matatu.

Thorsten Fink amesema kutokukata tamaa na mabao waliyofungwa katika kipindi cha kwanza ilikuwa ni sera yao na aliwaeleza suala hilo wachezaji wake wakati wa mapumziko.

Hata hivyo amedai kwamba walijiandaa vyema kabla ya mpambano huo wa jana ambapo alijua wanakwenda kupambana na timu nzuri na yenye kujua kulikabili lango la wapinzani.

No comments:

Post a Comment