KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, September 21, 2011

ARSENE WENGER AWAPIGA VIJEMBE WABAYA WAKE.

Baada ya ushindi wa mabao matatu kwa moja uliopatikana usiku wa kuamkia hii leo na kuifanya Arsenal kujipatia ushindi wake wa pili toka ulipoanza msimu huu wa ligi, meneja wa klabu hiyo Arsene Wenger amesema hana budi kukubaliana na yoyote anaempinga kwa sasa.

Arsene Wenger amesema anakubaliana na hali hiyo kutokana na mazingira yanayomzunguuka lakini ukweli bado anautambua yeye mwenyewe baada ya kuanza kuonekana kwa mafanikio ya kutinga katika hatua ya nne ya kombe la ligi.

Amesema wapo wengi waliotaka afukuzwe klabuni hapo kwa matokeo yaliyopatikana toka mwanzoni mwa msimu huu, lakini msimamo wa uongozi uliotolewa jana kupitia kwa mtendaji mkuu Ivan Gazidis umedhihirisha ni vipi bado anahitajika huko Emirates.

Katika mchezo wa jana wa hatua ya tatu ya kombe la ligi *Curling Cup* Arsenal walipata ushindi wa mabao matatu kwa moja baada ya kutanguliwa na wapinzani wao wanaocheza ligi daraja la pili Shrewsbury Town ambao walipata bao la kuongoza kupitia kwa James Collins katika dakika ya 16.

Arsenal walisawazisha bao hilo kupitia kwa beki wa pembeni Kieran Gibbs kabla ya Alex Oxlade-Chamberlain pamoja na Yossi Benayoun hawajaongezabao la pili na la tatu.

Kufuatia hatua hiyo Arsene Wenger amesema anaamini ushindi walioupata utawasaidia kurejea katika njia sahihi baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Blackburn Rovers kwa idadi ya mabao manne kwa matatu huku mchezo ujao ukitarajia kuwakutanisha na Bolton Wanderers siku ya jumamosi.

Arsene Wenger pia akasifia uwezo mkubwa ulionyeshwa na Alex Oxlade-Chamberlain.

No comments:

Post a Comment