KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, September 20, 2011

ARSENE WENGER YUPO KATIKA MIKONO SALAMA.

Mtendaji mkuu wa klabu ya Arsenal Ivan Gazidis amesisitiza jambo la uongozi wa klabu hiyo kutokua na papara za kumtimua kazi Arsene Wenger kufuatia mambo kumuendea kombo katika michezo ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza.

Ivan Gazidis amesisitiza jambo hilo baada ya kuulizwa na waandishi wa habari hii leo jijini London ambao walitaka kufahamu nini msimamo wa uongozi wa The Gunners dhidi ya Arsene Wenger ambae mpaka sasa amekishuhudia kikosi chake kikipata ushindi mara moja katika michezo mitano ya ligi msimu huu.

Amesema bado wanaamini kikosi cha Arsenal kinachoendelea kuhangaikia suala la kusaka ushindi kwa sasa kitasimama chini ya meneja huyo kutoka nchini Ufaransa na hakuna mpango wowote wa kumtimua kazi kama inavyodhaniwa na wengi.

Kiongozi huyo amedai kwamba kwa mtazamo wa hivi sasa, kikosi cha Arsenal bado kina nafasi kubwa ya kurejea katika ushindani na kama ingekuwa michezo ya ligi inaelekea ukingoni basi uwezekano mkubwa wa mzee Arsene Wenger kutupiwa virago vyake ungekuwepo.

Wakati huo huo Arsene Wenger amelazimika kusema sababu zinazopelekea wachezaji wake kutokufanya vizuri mwanzoni mwa msimu huu baada ya safu yake ya ulinzi kuruhusu magoli 13 katika michezo sita waliyocheza.

Amesema sababu kubwa inayopelekea tatizo hilo ni udhaifu wa safu yake ya ulinzi ambayo inakosa umakini, mawasiliano pamoja na ushirikiano hatua mbayo inapelekea wahusika kutokua kitu kimoja.

Hata hivyo amedai kwamba katika mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Blackburn Rovers mabao mawili waliyofungwa kutokana na Alex Song na Laurent Koscielny kujifunga wenyewe yalichangia kwa kiasi kikubwa kuwapoteza wachezaji wengine katika hali ya mchezo.

Lakini pamoja na kutoa sababu hizo mzee huyo wa kifaransa ameendelea kutanabai kwamba mafanikio yao msimu huu yatategemea na jinsi watakavyokabiliana na makosa yaliyojitokeza katika michezo waliyocheza.

Usiku huu Arsenal wanakabiliwa na mchezo wa hatua ya tatu ya michuano ya kombe la ligi ambapo watawakaribisha nyumbani Emirates Stadium Shrewsbury Town na baada ya mpambano huo mwishoni mwa juma hili watakua nyumbani wakicheza na;

• 24 Sept - Bolton (h)
• 2 Oct - Tottenham (a)
• 16 Oct - Sunderland (h)
• 23 Oct - Stoke (h)
• 29 Oct - Chelsea (a)

No comments:

Post a Comment