KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, September 20, 2011

Hernández Balcázar Chicharito KUREJEA UWANJANI KESHO.

Mabingwa wa soka nchini Uingereza Man Utd hii leo wamepokea taarifa njema kutoka kwa wakala wa mshambuliaji Javier Hernández Balcázar Chicharito ambae alipata dhoruba la kuchezewa rafu mbaya na beki wa pembeni wa Chelsea Ashley cole mwishoni mwa juma lililopita pale klabu hizo zilipokutana.

Eduardo Hernandez, wakala wa mshambuliaji huyo kutoka nchini Mexico amesema Javier Hernández Balcázar Chicharito kesho atarejea mazoezini baada ya jeraha lake kuendelea vyema na kuonyesha uharaka wa kupona mbali na ilivyotarajiwa.

Eduardo Hernandez, amesema kila mmoja alishutushwa na kitendo cha rafu aliyochezewa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kwa kudhani huenda ingemchukua muda mrefu kuwa nje ya uwanja, lakini kwa hivi sasa wanamshukuru mungu kwa maendeleo mazuri yanayoonekana.

Hata hivyo amedai kuwa licha ya kumtarajia kurejea mazoezini, anaamini Javier Hernández Balcázar Chicharito, atakuwa miongoni mwa wachezaji watakaojumuishwa kikosini katika mchezo wa mwishoni mwa juma hili dhidi ya Stoke City.

Kama itakumbukwa vyema meneja wa Man Utd Sir Alex Ferguson mara baada ya mchezo dhidi ya Chelsea alionyesha hofu ya kumkosa mshambuliaji huyo kwa muda wa majuma mawili yajao ama zaidi ya hapo.

No comments:

Post a Comment