KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, September 9, 2011

BADO NINA UAMINIFU KWA TORRES.

Mshambuliaji Fernando Torres bado anaendelea kupewa nafasi ya kutimiza azma ya kupachika mabao zaidi kama alivyokua na klabu ya Liverpool ambayo ilimsajili akitokea Atletico Madrid ya nchini kwao Hispania.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, ameendelea kupewa nafasi hiyo na meneja wa Chelsea Andre Villas-Boas ambapoa mesema bado anaamini Fernando Torres ana kila sababu za kufanya makubwa kama ilivyokua siku za nyuma.

Amesema mbali na watu wengi kumponda kutokana na kupachika bao moja mpaka sasa toka alipojiunga na Chelsea akitokea Liverpool mwanzoni mwa mwaka huu kwa ada ya uhamisho wa paund million 50, yeye binafsi anasadiki kusema Torres ni mshambuliaji mzuri miongoni mwa washambuliji mahiri duniani kote.

Kama itakumbukwa vyema Fernando Torres alifanikiwa kufunga bao hilo pekee katika mchezo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza dhidi ya West Ham Utd ambapo katika mchezo huo wagonga nyundo wa London walioporomoka daraja walikubali kisago cha matatu kwa sifuri.

No comments:

Post a Comment