KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, September 10, 2011

David Moyes APASUA UKWELI WA KUMUUZA ARTETA.

Meneja wa Everton David Moyes amesema alilazimika kumuuza Mikel Arteta katika kipindi cha usajili kilichofikia kikomo usiku wa kuamkia Septemba mosi baada ya kulazimishwa kufanya hivyo na mabosi wake.

Moyes amesema ulazima huo ulikuja kutokana na ukata wa fedha uliokua unaukabili uongozi wa The Toffees ambao ulitamani kuwasajili wachezaji lakini ulishindwa kufanya hivyo kutokana na sababu za kutokua na pesa za kutosha.

Amesema mara kadhaa alikua na mazungumzo na mwenyekiti wa Everton Bill Kenwright kwa ajili ya kutaka kufahamu nini mipango ya klabu hiyo katika suala la usajili lakini jibu alilokua anaambulia ni ulazima wa kuuza wachezaji ili wafanikishe suala hilo.

Hata hivyo meneja huyo kutoka nchini Scotland ameongeza kwamba Mikael Arteta pia alikua ameshaonyesha nia ya kutaka kuondoka klabuni hapo kwa kutaka kucheza michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya hivyo ilikua rahisi kwake kumuuza huko Emirates.

Katika hatua nyingine mashabiki wa Everton wameripotiwa kuwa na mikwaruzano na bodi ya viongozi wa klabu hiyo kutokana na kushindwa kufanya usajili wa uhakika ambao ungekisaidia kikosi chao kufanya vizuri msimu huu.

Mshabiki hao hii leo walipanga kuushurutisha uongozi kutoa sababu muhimu za kushindwa kufanya usajili kabla ya mchezo wa ligi dhidi ya Aston Villa ambao walizuklu huko Goodson Park.

No comments:

Post a Comment