KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, September 20, 2011

Breno Rodrigues Borges NUSURA AKUMBWE NA UMAUTI.

Beki kutoka nchini Brazil na klabu ya Bayern Munich Breno Rodrigues Borges ameazwa hospitalini nchini Ujerumani baada ya kuathiriwa na moshi mkali uliotanda katika nyumba yake ambayo ilishika moto na kuteketea kabisa.

Jeshi la polisi nchini Ujerumani limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ya moto na hali ya beki huyo inaendelea vizuri.

Taarifa iliyotolewa na jeshi la polisi nchini humo imeeleza kuwa, wakati nyumba ya Breno iliposhika moto hakukuwa na mtu mwingine yoyote zaidi yake.

Hata hivyo jeshi hilo la polisi limedai kwamba bado linaendelea kufanya uchunguzi wa kina kwa lengo la kufahamu chanzo cha moto huo, na watakapo maliza watatoa maelezo kamili kwa kile kilichopelekea ajali hiyo kutokea.

Breno ambae kwa sasa ana umri wa miaka 21, alijiunga na Bayern Munich akiwa na umri wa miaka 18, akitokea nyumbani kwao Brazil katika klabu ya Sao Paolo.

Mpaka sasa ameshaitumikia klabu hiyo ya Allianze Arena katika michezo 21, na bado hajabahatika kufunga bao.

No comments:

Post a Comment