KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, September 19, 2011

KIZAA ZAA CHA KADI NYEKUNDU YA IVAN KLASNIC.

Meneja wa Bolton Wanderers Owen Coyle amesema hakuna sababu ya kuomba radhi kwa niaba ya mshambuliaji Ivan Klasnic, ambae alionekana akimpiga kwa makusudi beki wa Norwich City Marc Tierney katika mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita.

Owen Coyle amesema hakuna haja ya kufanya hivyo kutokana na mazingira ya mchezo yalivyokua ambapo tayari muamuzi Howard Webb alishamuadhibu kwa kumuonyesha kadi nyekundu kutokana na kosa hilo.

Amesema licha ya kuonyeshwa kadi nyekundu, bado Ivan Klasnic hakustahili kuadhibiwa kwa namba hiyo kutokana na tukio hilo lilivyojitokeza ambapo ilionekana alimgonga Marc Tierney kwa bahati mbaya alipokua katika harakati za kugeuka.

Hata hivyo amedai kuwa muamuzi Howard Webb alikua hafahamu kilichoendelea lakini muamuzi wa pembeni alipotakiwa kutoa maelezo alitoa maelezo tofauti na mwishowe mchezaji wake alionyeshwa kadi nyekundu ambayo anaendelea kuipinga.

Katika mchezo huo Bolton Wanderers ambao walikua nyumbani huko reebok Stadium walikubali kichapo cha mabao mawili kwa moja kutoka kwa Norwich City.

No comments:

Post a Comment