KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, September 16, 2011

Cesc Fabregas AKANA KUISEMEA MBOVU ARSENAL.

Kiungo alieihama klabu ya Arsenal katika kipindi cha usajili kilichopita Francis Cesc Fabregas amesema hakufanya mahojiano na chombo chochote cha habari yaliyohusiana na safari yake ya kutoka nchini Uingereza hadi nchini Hispania.

Francis Cesc Fabregas amekanusha mpango huo wa kufanya mahojiano baada ya taarifa yake kutokewa katika baadhi ya vyombo vya habari vya nchini Uingereza ambavyo vilidai ameikashifu Arsenal kwa kusema klabu hiyo itasubiri sana kutwaa ubingwa kutokana na umahiri wa vikosi vya klabu kama Man Utd, Man city pamoja na Chelsea.

Amesema anatambua huenda mpango huo umepangwa na baadhi ya watu wasiomtakia mema katika maisha yake mara baada ya kudoka jijini London lakini bado akaendelea kushikilia msimamo wake wa kutosema maneno hayo.

Amesema anaamini mashabiki wa Arsenal wamekasirishwa na kile walichokiona ama kukisikia katika vyombo vya habari, lakini wanastahili kuwa watulivu na kutambua hakufanya na wala hatothubutu kufanya mpango wowote wa kuitusi The Gunners.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 ametanabai kwamba aliishi vyema na mashabiki, viongozi pamoja na wachezaji wa Arsenal na kuondoka kwake klabuni hapo kunastahili kuchukuliwa kama sehemu ya maisha yake na si uadui kama inavyoonekana kwa baadhi ya watu wasiomtakia mema.

Francis Cesc Fabregas aliihama Arsenal baada ya kuitumikia kwa muda wa miaka minane iliyopita na kwa kipindi chote hicho alifanikiwa kucheza michezo 212 na kupachika mabao 35.

Wakati huo huo ligi kuu ya soka nchini hispania kesho inaendelea tena ambapo:

Estadio El Molinón.
Sporting Gijón v Valencia CF

Nuevo Los Cármenes.
Granada CF v Villarreal CF

Iberostar Estadi
RCD Mallorca v Málaga CF

Camp Nou.
FC Barcelona v Osasuna

Estadio Ramón Sánchez Pizjuan.
Sevilla FC v Real Sociedad

No comments:

Post a Comment