KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, September 22, 2011

Petr Cech YUPO SALAMA.

Hali ya kipa wa klabu ya Chelsea Petr Cech inaendelea vizuri baada ya kukimbizwa hospitali kufuatia kugongana na mshambuliaji wa Fulham Orlando Sa katika mpambano wa usiku wa kuamkia hii leo wa kuwani ubingwa wa kombe la ligi *Curling Cup*.

Meneja wa klabu ya Chelsea Andre Villas-Boas amesema kipa huyo mwenye umri wa miaka 29 yupo katika mikono salama tofauti na wengi walivyokua wanafikiri huenda alipata maumivu makali mara baada ya kutokea kwa mgongano kati ya Sa.

Amesema endapo hali yake itaendelea kuridhisha na pengine kupona kabisa, huenda akamchezesha katika mchezo wa mwishoni mwa juma hili ambapo Chelsea watarejea katika uwanja wa nyumbani Stamford Bridge kupambana na Swansea City.

Katika hatua nyingine Andre Villas-Boas amesifia uwezo wa wachezaji wake ulioonekana jana dhidi ya Fulham ambao walitupwa nje ya michuano ya kombe la ligi kwa changamoto ya mikwaju ya penati baada ya kwenda sare ya bila kufungana katika muda wa dakika 120.

Amesema kiujumla walicheza vizuri na mara kadhaa walionekana kuwakabili vilivyo Fulham lakini umakini na mbinu tofauti za klabu hiyo inayonolewa na Martin Jol, zilichangia kuwapa upinzani mkali na kufikia hatua ya kupigiana mikwaju ya penati.

Katika mchezo huo Fulham itawalazimu wajilaumu wenyewe baada ya Pajtim Kasami kukosa mkwaju wa penati ndani ya muda wa kawaida ambao uliwaacha Chelsea wakicheza pungufu baada ya beki kutoka nchini brazil Alex kuonyeshwa kadi nyekundu.

No comments:

Post a Comment