KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, September 2, 2011

Craig Bellamy AFURAHIA KURUDI LIVERPOOL.

Kiungo mtukutu kutoka nchini Wales alirejea Anfield baada ya kuuzwa miaka minne iliyopita Craig Bellamy ameshindwa kuficha furaha yake ya kuzungumzia hatua ya kurejeshwa kundini na meneja wa sasa King Kenny Dalglish akitokea Man city.

Craig Bellamy ameelezea furaha yake kupitia televisheni ya klabu ya Liverpool ambapo amesema, ni hatua nzuri kwake kuwa mikononi mwa wana Liverpool na anaamini mchango wake yeye kama mchezaji utalisaidia jogooo la jiji.

Amesema huenda maisha yake ya soka yalikua yanelekea ukingoni kutokana na mazingira aliyokutana nayo mara baada ya kuondoka Anfield lakini amedai kuwa changamoto alizokutana nazo zimemfunza na pengine kesho na kesho kutwa litakua somo kwa wachezaji wengine.

Katika hatua nyingine kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32 amedai kuwa na hamu ya kutwaa vikombe mbali mbali akiwa na klabu hiyo na kwa mtazamo wa kikosi cha Liverpool kwa sasa amedai hatua hiyo iwezekana.

No comments:

Post a Comment