KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, September 8, 2011

Craige Bellamy ALISTAHILI KURUDI ANFIELD.

King Kenny Dalglish ametetea maamuzi yake ya kumrejesha kundini kiungo mshambuliaji kutoka nchini Wales Craig Bellamy akitokea Man city ambapo alikosa muelekeo baada ya kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo ya Etihad Stadium.

King Kenny Dalglish amesema mchezaji huyo bado ana uwezo mkubwa wa kucheza soka na anaamini kurejea kwake Anfiled kutakisaidia kikosi chake kufikia malengo yaliyowekwa msimu huu, ambayo yameazimia kuvunja mwiko wa kumaliza bila kupata ubingwa wa michuano watakayoshiriki.

Amesema Craige Bellamy alikuwa katika wakati mgumu wa kuonyesha uwezo wake akiwa na Man City, lakini hivi sasa atatimiza lengo lake la kucheza kila juma kutokana na kutarajia kumpa nafasi ya kucheza kama matarajio yake yanavyomtuma.

Hata hivyo amemshukuru mchezaji huyo kwa kukubali kujitoa muhanga kwa kuliafiki suala la kulipwa mshahara wa paund 80,000 kwa juma tofauti na alivyokua akilipwa Etihad Stadium ambapo alikua akipokea kiasi kikubwa zaidi ya hicho.

Siku moja baada ya kusajiliwa klabuni hapo Craige Bellamy alielezea furaha yake ya kurejea tena Anfield huku akieleza mipango na matarajio aliyojiwekea kutokana na muonekano wa kikosi cha The Reds msimu huu.

No comments:

Post a Comment