KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, September 19, 2011

Davide Santon AZUSHA HOFU KUBWA ST JAMES PARK.

Hofu imetanda kwa viongozi wa benchi la ufundi kufuatia hatua ya kuumia kwa beki wa pembeni ambae alijiunga na Newcastle Utd akitokea kwa mabingwa wa soka duniani Inter Milan Davide Santon.

Hofu hiyo imetawala kwa viongozi wa becnhi la ufundi wa klabu hiyo kufuatia maumivu ya goti yanayomkabili beki huyo mwenye umri wa miaka 20 aliyoyapata mwishoni mwa juma lililopita akiwa katika maandalizi ya mchezo wa ligi dhidi ya Aston Villa ambao ulimalizika kwa matokeo ya sare ya bao moja kwa moja.

Meneja wa Newcastle Utd Alan Pardew amesema hii leo Davide Santon alilazimika kupelekwa jijini London kwa ajili ya kufanyiwa matibabu zaidi na tayari wameshaelezwa huenda ikamchuku majuma manne kurejea tena uwanjani.

Amesema bado hawajafahamu kama atafanyiwa upasuaji lakini majibu ya haraka waliyoyapata huenda Davide Santon akakaa nje ya uwanja kwa muda wa majuma manne na endapo atalazimika kufanyiwa upasuaji hawatokua na hiyana na suala hilo zaidi ya kujipoanga kivingine.

Kuumia kwa beki huyo mwenye umri wa miaka 20 bado kunaendelea kumpa wakati mgumu Alan Pardew kupanga vyema kikosi chake ambapo katika mchezo uliopita dhidi ya Aston Villa alilazimika kumtumia Ryan Taylor kama beki wa upande wa kushoto.

Hata hivyo bado inadhaniwa huenda Ryan Taylor akaendelea kutumika katika upande wa kushoto katika mchezo wa hatua ya tatu ya kuwania kombe la ligi *Carling Cup* dhidi ya Nottingham Forest ambao watakuwa nyumbani huko City Ground hapo kesho.

Davide Santon alisajiliwa klabuni hapo kama mbadala wa Jose Enrique alieihama Newcastle Utd na kujiunga na Liverpool mwanzoni mwa mwezi uliopita.

No comments:

Post a Comment