KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, September 19, 2011

LUCA MODRIC NA ADEBAYOR WAMKUNA BABU.

Baada ya ushindi wa mabao manne kwa sifuri dhidi ya majogoo wa jiji Liverpool, meneja wa Tottenham Hotspurs Harry Redknapp amemtaka mwenyekiti wa klabu hiyo Daniel Levy kufanya mipango ya kuzungumza na kiungo kutoka nchini Croatia Luka Modric juu ya masuala ya kusaini mkataba mpya.

Harry Redknapp ameonyesha nia ya kuona suala hilo linafanyika haraka iwezekanavyo baada ya kufurahishwa na uwezo wa kiungo huyo aliouomnyesha katika mpambano wa jana huku akifunga bao la kwanza kwa shuti kali.

Amesema kwa sasa Luka Modric amerejea katika hali yake ya kawaida na ana imani amerejesha mapenzi na Spurs hivyo utakuwa ni wakati mzuri wa kufanya nae mazungumzo ili aweze kusaini mkataba mpya ambao utaendelea kumuweka huko White Hart lane.

Licha ya kutaka kutumia nafasi hiyo, pia Harry Redknapp anahofia endapo suala hilo la mazungumzo halitotiliwa maanani kwa hivi sasa huenda Luca Modric akaondoka mwezi januari kwa kusajiliwa na klabu ya Chelsea ambayo ilikua mstari wa mbele kutaka kumsajili katika kipindi cha usajili kilichofikia tamati usiku wa kuamkia September mosi.

Chelsea tayari alionyesha nia ya kumuhitaji kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25 kwa udi na uvumba na kufikia wakati walikua tayari kutoa kiasi cha paund million 40 kama ada ya uhamisho wake kutoka kaskazini hadi magharibi mwa jiji la London.Katika hatua nyingine Harry Redknapp amekiri kufurahishwa na uwezo wa mshambuliaji kutoka nchini Togo Emmanuel Sheyi Adebayor ambae amemsajili kwa mkopo akitokea Man City ambako alikua na wakati mgumu wa kuwanai nafasi katika kikosi cha kwanza.

Harry Redknapp amesema hatua ya mshambuliaji huyo kufunga mabao mawili kati ya manne yaliyowapa ushindi katika mchezo wa jana anaamini itaendelea kumjengea mahusiano mazuri na mashabiki wa Spurs ambao siku za nyuma walimchukia kutokana na kadhia aliyokua anawapa akiwa na timu pinzani.

No comments:

Post a Comment