KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, September 2, 2011

Diego Ribas da Cunha KUANZA MAISHA HISPANIA.

Uongozi wa Atletico Madrid hii leo umemtambulisha rasmi kiungo kutoka nchini Brazil, Diego Ribas da Cunha kuwa mchezaji halali wa klabu hiyo, huku zikiwa zimepita siku mbili baada ya dirisha la usajili kufungwa.

Diego Ribas da Cunha ametambulishwa kwa waandishi wa habari pamoja na kwa mashabiki wa Atletico Madrid, baada ya kukamilisha uhamisho wake kimya kimya akitokea kwenye klabu ya Wolfsburg, ya nchini Ujerumani kwa mkopo.

Kabla ya kutambulishwa hii leo, mashabiki pamoja na vyombo vya habari viliripoti taarifa za kusajiliwa kwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26, pasipokua na uhakika wa asiliamia mia moja, na hii ilitokana na ukimya wa usajili wake uliofanyika usiku wa kuamkia Septemba mosi.

Meneja wa Atletico Madrid Gregorio Manzano amesema kusajiliwa kwa kiungo huyo kunaendelea kudhihirisha wazi mipango yake ya kufanya vyema msimu huu ambao unatabiriwa kuwa na upinzani mkali kuliko misimu mingine iliyopita kutokana na maandalizi yaliyofanywa.

Amesema Diego Ribas da Cunha ni mchezaji anakwenda sambamba na mfumo anaoutumia klabuni hapo, hivyo anaamini atamsaidia katika mikiki mikiki ya kuwania point tatu muhimu ima iwe nyumbani ama ugenini.

Nae Diego Ribas da Cunha amesema kuondoka kwake nchini Ujerumani kumemfungulia ukurasa mpya wa maisha yake katika soka ambapo sasa anatarajia kupata changmoto tofauti ambazo zitaendeleza kipaji na uwezo wake anapokua uwanjani.

Diego Ribas da Cunha ameondoka Weder Bremen, huku akiacha mahusiano mabaya kati yake na meneja wa klabu hiyo Wolfgang-Felix Magath baada ya kumuengua katika kikosi chake kilichomalizia msimu uliopita hali iliyopelekea kiungo huyo kufikia hatua ya kujitenga na wenzake.

No comments:

Post a Comment