KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, September 27, 2011

Dimitar Ivanov Berbatov KUMALIZA UKAME WA MABAO LEO?

Mshambuliaji kutoka nchini Bulgaria Dimitar Ivanov Berbatov ambae ana ukame wa kufunga mabao katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa muda wa miaka miwili sasa, huenda akapewa nafasi ya kuanza katika kikosi cha Man Utd kitakachokua nyumbani usiku huu kupambana na FC Basel kutoka nchini Uswiz.

Dimitar Berbatov anategemea kupewa nafasi hiyo kufuatia mapungufu yaliyojitokeza katika kikosi cha kwanza cha Man Utd ambacho hakitakuwa na washambuliaji wake wawili Wayne Rooney pamoja na Javier Hernandez ambao wote kwa pamoja ni majeruhi.

Sir Alex Ferguson akiwa katika mkutano na waandishi wa habari amesema mshambuliaji huyo ana nafasi kubwa ya kucheza usiku huu huku akiamini huenda akamaliza ukame wa mabao unaomkabili toka mwaka 2008 ambapo bao lake la mwisho alifunga katika mchezo dhidi ya Celtic ya nchini Scotland.

Sir Alex Ferguson pia akawaondoa hofu mashabiki wa Man Utd kwa kusema hatau ya kutomchezesha mshambuliaji huyo ni ya kawaida na wala isichukuliwe anamtumia kama mchezaji kiraka zaidi ya kutambua bado ni halali kwa Man utd.

Man Utd usiku huu wanaingia uwanjani huku wakiwa na uchu wa kutaka kurekebisha makosa yao yaliyojitokeza katika mchezo wa kwanza wa kundi la tatu ambapo walilazimisha sare ya bao moja kwa moja dhidi ya Sport Lisboa Benfica.

Kwa upande wa FC Basle wao wamesafiri hadi nchini Uingereza huku wakikumbuka furaha ya ushindi wa mabao mawili kwa moja walioupata katika mchezo wao wa kwanza wa kundi la tatu dhidi ya Otelul Galati uliochezwa nchini Uswiz majuma mawili yaliyopita.

Michezo mingine ya ligi ya mabingwa barani ulaya itakayochezwa usiku huu ni pamoja na:

Luzhniki, Moscow
CSKA Moscow v Internazionale

Stadio San Paolo, Naples
Napoli v Villarreal CF

Hüseyin Avni Aker, Trabzon
Trabzonspor v Lille

Stade Gerland, Lyon
Olympique Lyon v Dinamo Zagreb

Estadio Stantiago Bernabéu, Madrid
Real Madrid v Ajax

No comments:

Post a Comment