KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, September 27, 2011

TAMBO KABLA YA GAME YA HII LEO.

Ukimya uliotawala kwa upande wa mabingwa wa zamani wa barani humo FC Bayern Munich umeendelea kutoa nafasi kwa wapinzani Man City kuzungumzia mchezo wa usiku huu utakaopigwa huko Allianze Arena mjini Munich.

Man city wameendelea kuuzungumzia mchezo huo ambapo kwa hii leo mshambuliaji kutoka nchini Bosnia Edin Dzeko, ametoa tahadhari kubwa kwa kusema watahakikisha wanavunja mwiko wa Fc Bayern Munich wa kutokufungwa katika michezo tisa ya msimu huu ambayo wameshacheza mpaka hivi sasa.

Edin Dzeko, amesema rekodi hiyo ya Fc Bayen munich ni nzuri na inapendeza lakini wao wamedhamiria kuivunja kwa kuwafunga nyumbani hasa ikizingatiwa katika mchezo uliopita wa kundi la kwanza walipata matokeo ya sare dhidi ya Società Sportiva Calcio Napoli kutoka nchini Italia.
Amesema kwa sasa kikosi chao kipo vizuri kufuatia usajili uliofanywa mwanzoni mwa msimu huu ambao umewajumuisha wachezaji wengi wenye uzoefu wa kucheza michuano mikubwa kama ya ligi ya mabingwa barani Ulaya huku akigusia ujio wa Samir Nasri alietokea Arsenal pamoja na Sergio Aguero walitokea Athletico Madrid.

Katika hatua nyingine Dzeko akatetea maamuzi yake ya kuikacha Fc Bayern Munich ambayo ilionyesha nia ya kutaka kumsajili mwezi januari msimu uliopita na mwishowe alikubali kuelekea mjini Manchester.

Kama itakumbukwa vyema hapo jana kiungo kutoka nchini Hispania David Silva nae alitamba kwa kusema kikosi cha Man City kinaelekea Allianze Arena usiku huu kwa lengo moja tu, la kuvunja ukuta wa Fc Bayern Munich.

Wakati huo huo beki kutoka nchini Ujerumani Jerome Boateng amesema ana shauku kubwa ya kukutana na kikosi cha Man City usiku huu kwa minajili ya kutaka kuuthibitishia ulimwengu nini kilichompelekea kuondoka Etihad Stadium na kujiunga na Fc Bayern Munich mwishoni mwa msimu uliopita.

Amesema ni furaha kubwa sana kwake kukutana na klabu hiyo ambayo ilikubali kumuachia kwa paund million 13.5 baada ya kuitumikia kwa msimu mmoja ambao hakupendezwa nao kufuatia maamuzi ya Roberto Mancini kumchezesha nafasi ya beki wa pembeni ili hali yeye binafsi alihitaji kucheza katika nafasi ya beki wa kati kati.

No comments:

Post a Comment