KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, September 7, 2011

Emmanuel Sheyi Adebayor KUITUMIKIA SPURS JUMA HILI.

Mshambuliaji kutoka nchini Togo Emmanuel Sheyi Adebayor mwishoni mwa juma hili anatarajia kuitumikia klabu ya Tottenham Hotspurs iliyomsajili kwa mkopo akitokea Man City katika kipindi cha usajili kilichofikia tamati usiku wa kuamkia Septemba mosi.

Emmanuel Sheyi Adebayor anatarajia kucheza mchezo wa mwishoni mwa juma hili ambapo Spurs watafunga safari hadi Molineux Stadium kwenda kucheza na wenyeji wao Wolverhampton Wanderers.

Meneja wa Tottenham Hotspurs, Harry Readknap amethibitsiha taarifa za kutarajia kumpa nafashi mshambuliaji huyo ambae aliwahi kuwatumikia mahasimu wakubwa huko kaskazini mwa jijini London Arsenal.

Amesema mshambuliaji huyo amerejea katika kiwango chake cha kawaida mara baada ya kupelekwa kwa mkopo Real Madrid mwezi januari mwaka huu hivyo anaamini matarajio yake yatafanikiwa kupitia kwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27.

Hata hivyo Rednapp amesema hadhani kama upinzani uliopo kati yao na Arsenal utamzuia mshambuliaji huyo kuonyesha uwezo wake atakapokua uwanjani na pia akawazungumzi mashabiki wa Spurs kwa kusema anaamini hawatomchukia kwa sababu aliwahi kuwafunga akiwa na washika bunduki wa Ashbuton Grove pamoja na Real Madrid.

Amesema msimu uliopita alifanikiwa kumsajili William Gallas na alionyesha uwezo mkubwa tena mbele ya klabu hiyo ambayo aliitumikia kwa misimu minne akitokea Chelsea.

No comments:

Post a Comment