KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, September 7, 2011

Samson Siasia ATOA VISINGIZIO KIBAO !!

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Nigeria, Samson Siasia amesema haoni sababu wa kuwataka radhi mashabiki wa soka nchini humo kufuatia kichapo cha mabao matatu kwa moja walichokipokea jana kutoka kwa Argentina.

Samson Siasia amesema hawezi kufanya hivyo zaidi ya kuwapongeza wachezaji wake kwa kazi waliyionyesha jana, huku akitoa sababu za kupoteza mchezo huo kwa kusema kikosi chake kilikua kimechoka kutokana na mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita.

Amesema kila mmoja nchini Nigeria anatambua timu ya taifa ya nchi hiyo ilikua katika jukumu zito la mchezo wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya barani afrika za mwaka 2012 dhidi ya Madagascar ambao walikubali kichapo cha mabao mawili kwa sifuri.

Samson Siasia pia akatanabai kwamba mara baada ya mchezo huo walisafiri moja kwa moja hadi nchini Bagladesh kwa muda wa saa 14, hivyo walifika wakiwa wamechoka.

Hata hivyo kocha huyo amedai kwamba mchezo kwa ujumla ulikua mzuri, na amefurahishwa na kitendo cha kucheza na timu ya taifa ya Argentina iliyokamilika tena kwa kuchagizwa na manjonjo ya mchezaji Lionel Messi ambae alionekana kuwa tishio dhidi ya kikosi chake.

Katika mchezo huo mabao ya timu ya taifa ya Argentina yalipachikwa wavuni na Gonzalo Higuen, Angel Di Maria pamoja na Elderson aliejifunga mwenyewe huku bao la kufutia machozi la Nigeria likifungwa na Chinedu Obasi.

No comments:

Post a Comment