KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, September 16, 2011

Gian Piero Gasperini YUPO KATIKA MIKONO SALAMA.

Raisi wa klabu bingwa duniani Internazionale Milano Massimo Moratti amekanusha taarifa za kujipanga kumtimua kazi meneja wa klabu hiyo Gian Piero Gasperini kufuatia kuanza vibaya msimu wa mwaka 2011-12.

Massimo Moratti ametoa msimamo huo kufuatia minong’ono inayoendelea katika vyombo vya habari nchini Italia ambayo inadai Gian Piero Gasperini yu njiani kutimuliwa baada ya kushindwa kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Massimo Moratti amesema kibarua cha Gian Piero Gasperini bado kipo katika mikono salama na wao kama viongozi wanaridhishwa na kazi yake anayoifanya mpaka sasa.

Amedai kupoteza mchezo wa ufunguzi wa ligi ya nchini Italai dhidi ya Parlemo walioibuka na ushindi wa mabao manne kwa matatu pamoja na kupoteza point tatu za mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya Trabzonspor, kwao imekua fundisho na anaamini makosa yaliyojitokeza yatatumika kama changamoto katika mchezo wa mwishoni mwa juma hili dhidi ya AS Roma.

Katika hatua nyingine kiungo kutoka nchini Serbia Dejan Stankovic yupo katika mashaka makubwa ya kuukosa mchezo dhidi ya AS Roma, huku kiungo mchezeshaji kutoka nchini Uholanzi Wesley Sneijder akionyeasha matumaini ya kupona maumivu ya kifundo cha mguu.

Wakati Inter Milan wakitarajia kurejea uwanjani kesho, hii leo ligi ya nchini Italia inaendelea kwa kupigwa mchezo mmoja ambapo:

Stadio Sant'Elia,
Cagliari Vs Novara

No comments:

Post a Comment