KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, September 9, 2011

Harry Redknapp ATANGAZA VITA YA KUMTAKA BECKS.

Siku moja baada ya meneja wa QPR Nail Warnock kuthibitisha huenda akamsajili kiungo kutoka nchini humo David Beckham, hii leo meneja wa Tottenham Hotspurs Harry Redknapp amesema angependa kumpelekea mchezaji huyo White Hart lane utakapofika mwezi January mwaka 2012.

Harry Redknapp ametangaza hatua hiyo kwa kusema endapo David Beckham ataonyesha ni ya kutaka kuitumikia Spurs pindi atakapomaliza mkataba wake na klabu ya Los Angel Galax ya nchini Marekani hatokua na hiyana ya kumpokea katika utawala wake.

Amesema mchezaji huyo licha ya kuwa na umri wa miaka 36, bado ana uwezo mkubwa wa kucheza soka na endapo atatimiza matarajio ya kuwa nao atapeleka mabadiliko makubwa ndani ya kikosi cha Spurs kutokana na uzoefu alio nao.

Uongozi wa Tottenham Hotspurs, ulishawahi kuonyesha nia ya kutaka kumsajili kwa mkopo David Beckham lakini mpango huo uliingia dosari mara baada ya kuumia kisigino kabla ya fainali za kopmbe la dunia zilizofanyika nchini Afrika kusini mwaka jana, hatua ambayo ilimchukua muda mrefu kurejea tena uwanjani.

Msimu uliopita David beckham alipata nafasi ya kufanya mazoezi sanjari na wachezaji wa Spurs hatua mbayo ilizua minong’ono miongoni mwa mashabiki ambayo ilidai huenda alitaka kusajiliwa kwa mkopo na klabu hiyo ya kaskazini mwa jijini London.

No comments:

Post a Comment