KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, September 9, 2011

Jose Mourinho AIKATAA OFA YA KUWA MENEJA TAJIRI DUNIANI !!

Meneja wa klabu ya real Madrid Jose Mourinho ameripoptiwakukataa ofa ya kukifundisha kikosi cha klabu ya Anzhi Makhachkala ya nchini urusi ambayo ingemfanya kuwa meneja anaelipwa mshahara mkubwa kuliko mameneja wote duniani.

Taarifa zilizochapishwa na gazeti la The Marca la nchini Hispania zimeeleza kwamba meneja huyo kutoka nchini Ureno amekataa ofa hiyo ambayo ingempa nafasi ya kulipwa mshahara wa paund million 22 kwa mwaka baada ya kukatwa kodi.

Gazeti hilo limeendela kueleza kwamba mmiliki wa klabu ya Anzhi Makhachkala Suleyman Kerimov, alipania kumuajiri kazi Jose Mourinho kwa kuamini kwamba huenda mipango ya kufikia malengo aliyojiwekea msimu huu ingetimia kwa haraka.

Hata hivyo taarifa hizo zimeeleza kwamba tajiri huyo alianza kuonyesha nia ya kutaka kumuajiri Mourinho toka mwezi januari mwaka huu, na kwa kipindi chote hicho amekua akishindwa kutimiza ndoto zake.

Katika kuonyesha ni vipi mmiliki huyo alivyokua na uchu wa kuona klabu yake inapata mafanikio nchini Uruisi pamoja na barani ulaya, tayari ameshakamilisha mipango ya kuwasajili wachezaji kama Yuri Zhirkov akitokea Chelsea, beki mkongwe kutoka nchini Brazil Roberto Carlos, pamoja na mshambuliaji kutoka nchini Cameroon Samuel Eto'o ambae amekua mchezaji anaelipwa mshahara mkubwa kwa juma kuliko wachezaji wote duniani.

No comments:

Post a Comment