KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, September 26, 2011

KUISAIDIA ARSENAL KWANZA MAMBO MENGINE BAADAE.

Mshambuliaji kutoka nchini Uholanzi na klabu ya Arsenal Robin van Persie amesema hana pupa ya kutaka kusaini mkataba mpya na klabu hiyo na badala yake anafikiria ni vipi atakavyoweza kuisaidia The Gunnes kufikia malengo yake msimu huu.

Robin van Persie ambae alifunga bao la 100 katika mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Bolton Wanderers amesema suala la kusaini mkataba mpya kwa sasa halipi umuhimu mkubwa kutokana na muonekano wa kikosi chao ambacho kimeanza vibaya msimu huu lakini kwa sasa kinaonyesha muelekeo mzuri.

Amesema yapo mengi ya kufanya huko Emirates na suala la kuanza mazungumzo ya kusaini mkataba mpya litafuata na katu hawezi kuyapa nafasi masuala hayo mawili kwa wakati mmoja.

Tayari mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 ameshaanza kuhusishwa na taarifa za kuwa mbioni kuikacha Arsenal pindi mkataba wake utakapofikai kikomo huku ikisemekana hatua hiyo huenda ikajitokeza kufuatia kuchukizwa na maamuzi ya kuondoka kwa Cesc Fabregas pamoja na Samir Nasri, walioihama Arsenal mwanzoni mwa msimu huu.

Katika hatua nyingine meneja wa Arsenal Arsene Wenger amekaririwa na vyombo vya habari akitoa kauli kama ya Robin Van Parsie ambapo amesema hakuna haraka ya kuanza mazungumzo ya kumtaka mshambuliaji huyo kusiani mkataba mpya.

Amesema malengo yake kwa sasa ni kuhakikisha wanakaa sawa katika uwiyano wa kupata ushindi kwenye michezo inayowakabili na kisha masuala mengine ya yatafuata huku akiahidi kulitimiza jukumu la mkataba wa Van Parsie kadri awezavyo.

Mkataba wa Robin Van Parsie unatarajia kufikia kikomo mwishoni mwa msimu ujao, hatua ambayo huenda ikampa nafasi ya kuanza kunyemelewa na klabu nyingine za ndani na nje ya nchini Uingereza.

No comments:

Post a Comment