KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, September 26, 2011

TUPO TAYARI KUUANGUSHA UKUTA WA BAYERN MUNICH.

Kiungo kutoka nchini Hispania David Silva amesisistiza jambo la kikosi cha Man City kwenda nchini Ujerumani kwa lengo la kuuangusha ukuta wa mabingwa wa zamani wa barani Ulaya FC Bayern Munich ambao kesho watakua nyumbani Allianze Arena katika mchezo wa kundi la kwanza la michuano ya ligi ya mabingwa barani humo.

David Silva ametoa msisistizo huo huku akifahamu fika mchezo wa kesho utakua na kila aina ya upinzani kutokana na mazingira ya vikosi vya pande hizo mbili kuhitaji ushindi kwa namna yoyote ile.

Amesema kikosi chao kipo vizuri na hana shaka na mipango ilitopandaliwa na meneja Roberto Mancini ya kuhakikisha wanapata ushindi wa kwanza katika michuano ya ligi ya ambingwa barani ulaya ambayo katika mchezo wa kwanza ilishuhudia wakilazimishwa sare ya bao moja kwa moja dhidi ya Società Sportiva Calcio Napoli, huko Etihad Stadium majuma mawili yaliyopita.

Amesema hakuna asietambua ugumu wa Bayern Munich wanapokua katika michuano ya nyumbani kwao Ujerumani pamoja na muchuano ya nje ya nchini humo hivyo watakwenda wakilijua hilo lakini bado mipango ya ushindi itaendelea kuwepo kama ilivyopangwa.

Bayern Munich hiyo kesho wataingia uwanjani huku wakiwa na mpangilio mzuri wa kucheza kwa dakika 838 bila kufungwa huku wakichagizwa na uwepo wa wachezaji kama Jerome Boateng pamoja na Daniel van Buyten ambao wamewahi kuitumikia Man City.

Kwa upande wa Man city wao mpaka hivi sasa wameshaingia uwanjani mara sita toka msimu huu ulipoanza na bado hawajapoteza mchezo hata mmoja hali ambayo inaendelea kudhihirisha wazi kwamba mpambano huo wa kesho utakua na kila sababu za upinzani.

Mchezo mwingine katika kundi hilo la kwanza ambao utachezwa kesho ni kati ya Società Sportiva Calcio Napoli dhidi ya Villareal.

No comments:

Post a Comment