KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, September 26, 2011

MAN UTD KUWAKOSA WANANE KESHO.

Kikosi cha Man Utd kesho kitakuwa nyumbani kikiendelea na michezo ya ligi ya mabingwa barani ulaya huku kikiwa na mapungufu ya kuwakosa wachezaji wanane wa kikosi cha kwanza ambao kwa sasa ni majeruhi.

Meneja wa klabu hiyo Sir Alex Ferguson amethibitisha kutokuwepo kwa wachezaji hao wanane ambapo amesema licha ya mapungufu hayo bado ana amini wana nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi dhidi ya FC Basle kutoka nchini Uswiz.

Amesema miongoni mwa wachezaji hao majeruhi yupo mshambuliaji wake kutoka nchini Ungereza Wayne Rooney alieumia katika mchezo uliopita pamoja na Javier Hernandez Balcazer Chicharito ambae bado anasumbuliwa na maumivu ya ugoko aliyoyapata katika mchezo dhidi ya Chelsea majuma mawili yaliyopita.

Kutokuwepo kwa washambuliaji hao kunatoa nafasi kwa Sir Alex Ferguson kufanya chaguo la kuwatumia washambuliaji wawili kati ya Michael Owen, Dimitar Berbatov ama Danny Welbeck ambae kwa sasa amerejea katika hali yake ya kawaida.

Wachezaji wengine ambao hawatokuwepo kikosini hiyo kesho ni mabeki wa kati kama Jonny Evans (maumivu ya kifundo cha mguu), Chris Smalling (maumivu ya nyonga) pamoja na Nemanja Vidic (maumivu ya kiazi cha mguu).

Wengine ni viungo ambao ni Tom Cleverley pamoja na Darron Gibson.

No comments:

Post a Comment