KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, September 13, 2011

NITAPANGA KIKOSI KWA JUHUDI ZA WACHEZAJI - AVB.

Meneja wa klabu ya Chelsea Andre Villas-Boas ameendelea kutetea mpango wake wa kumuweka nje mshambuliaji kutoka nchini Hispania Ferdinand Torres katika mpambano wa usiku huu wa ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya Bayer-Leverkusen toka nchini Ujerumani.

Andre Villas-Boas amesema maamuzi ya kucheza ama kutokucheza kwa mshambuliaji huyo yapo mikononi mwake na hadhani kama kuna mwingine anaweza kumuingia katika maamuzi atakayoyafanya katika upangaji wa kikosi kitakachofungua michuano ya ligi ya mabingwa huko Stamford bridge.

Amesema hata kama mchezaji atachukizwa na maamuzi hayo bado anastahili kutambua kwamba kila mmoja ndani ya Chelsea anastahili kucheza kutokana na uwezo wake anaouonyesha uwanjani hivyo ni jukumu la muhusika kuonyesha bidii pale itakapohitajika.

Shughuli ya kukosekana katika kikosi cha hii leo kwa Ferdinand Torres ilianza kudhihirika toka jana ambapo ilidaiwa huenda nafasi yake ikachukuliwa na mshambuliaji kinda Daniel Sturridge ambae alifanya vizuri katika mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Sunderland.

Katika hatua nyingine Andre Villas-Boas amewazungumzia wapinzani wao usiku huu Bayer-Leverkusen kwa kusema ni wazuri kutokana na uwezo wao wanapokua uwanjani na anaamini uwezo na uzoefu wa wachezaji wa klabu hiyo utawasaidia kujiamini dhidi ya kikosi chake.

Michael Ballack kiungo aliewahi kuitumikia Chelsea, ambae kwa sasa anakitumikia kikosi cha Bayer-Leverkusen amesema wanatambua wanakwenda kupambana na The Blues yenye mtazamo tofauti kutokana na ujio wa meneja mpya tena mwenye umri mdogo ambae ameshajizolea sifa kubwa barani Ulaya akiwa na FC Porto.

Wakati huo huo uongozi wa klabu ya Chelsea unafanya uchunguzi makini kufuatia kauli iliyotolewa mwishoni mwa juma lililopita na mshambuliaji Ferdinand Torres ambayo iliwaponda wachezaji wenzake kwa kusema viongo wa The Blues ni wazito na ndio maana wanashindwa kumuwezesha kupachika mabao.

Torres anadaiwa kutoka kauli hiyo alipokua nchini kwao Hispania huku akidai Andre Villas-Boas aliliona hilo na ndio maana akaharakisha kumsajili kiungo Juan Mata kutoka Valencia Fc.

No comments:

Post a Comment