KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, September 29, 2011

MFANYABIASHARA WA KIMAREKANI AWA RAISI WA AS ROMA.

Mfanya biashara kutoka nchini Marekani Thomas DiBenedetto ametangazwa kuwa raisi wa klabu ya AS Roma baada ya kukamilisha mipango ya kununua asilimia 67 ya hisa za klabu hiyo mwezi mmoja uliopita.

Thomas DiBenedetto anakuwa raisi wa 22 wa klabu hiyo ya mjini Roma, na sasa anaichukua kutoka mikononi mwa familia ya Sensi ambayo imekuwa madarakani kwa muda wa miaka 18 iliyopita.

Hatua za kutangazwa kwa mfanyabiashara huyo zimethibitishwa muda mchache baada ya masuala la kisheria kukamilishwa na mwanasheria wa benki UniCredit Roberto Cappelli ambae alipitia mipango yote ya kisheria na kuona haina doa kwa Thomas DiBenedetto.

Utaratibu wa kuthibitishwa na mwanasheria wa benki UniCredit, umekuja kufuatia Thomas DiBenedetto, kufanya kazi na benki hiyo kwa kipindi kirefu hatua ambayo ilipelekea kufanya mpango wa kuinunua AS Roma kwa uaminifu uliopo dhidi ya benki hiyo.

Kwa mantiki hiyo sasa Thomas DiBenedetto anakuwa raisi wa kwanza wa klabu ya AS Roma ambae si raia wa nchini italia pamoja na kuwa mmiliki wa klabu ya michezo katika ardhi ya nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment