KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, September 23, 2011

Owen Hargreaves AISEMEA MBOVU MAN UTD.

Jopo la madaktari la klabu bingwa nchini Uingereza Man utd, limelaumiwa na aliekua kiungo wa klabu hiyo Owen Hargreaves ambae kwa sasa anaitumikia klabu ya Man City iliyomsajili akiwa kama mchezaji huru mwezi August mwaka huu.

Owen Hargreaves ametoa lawama hizo kwa jopo la madaktari la Man Utd kwa kusema alipatiwa matibabu ya goti kwa kipindi kirefu bila kupona huku akiambulia maumivu makali ya sindano kila kukicha.

Amesema lengo lake lilikua ni kuhitaji kupona lakini alichomwa sindano kama nguruwe mwitu, hatua ambayo ilikua haimfurahishi hata kidogo kutokana na mafanikio ya kupona majeraha ya goti kutokuonekana kama ilivyokua inatarajiwa.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 30 ameendelea kutanabai kwamba licha ya kupatiwa matibabu hayo kwa kipindi kirefu bado alishangazwa na maamuzi ya kuachwa kwake licha ya kuuomba uongozi kuendelea kuwepo huko Old Trafford kwa kuitumikia Man utd kwa mkataba wa kutokulipwa kama ilivyo kwa wachezaji wengine.

Hata hivyo kauli hiyo ya Owen Hargreaves, imejibiwa na meneja wa Man Utd Sir Alex Ferguson alipokua katika mkutano na waandishi wa habari mapema hii leo ambapo amesema jopo la madaktari wa klabu hiyo linastahili kusifiwa kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa kiungo huyo.

Sir Alex Ferguson amesema kiungo huyo ana haki ya kuzungumza lolote lakini bado anatambua ukweli upo moyoni mwake.

Nae meneja wa Man City Roberto Mancini amesema kurejea uwanjani kwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31 ni sehemu nzuri ya kuanza upya maisha yake ya soka na hatopendezwa na kitendo cha kuzungumzwa na masuala yake yaliyopita zaidi ya kutazama mustakabali wake wa mbele.

Amesema kiungo huyo alipokelewa vyema huko Etihad Stadium na aliendelea kutazamwa kutokana na afya yake na kwa sasa wanafarijika kwa kumuona tena uwanjani baada ya kuumia mara kwa mara akiwa na Man Utd.

No comments:

Post a Comment