KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, September 23, 2011

TIMU YA TAIFA YA IRAQ YAPIGWA MARUFUKU.
Shirikisho la soka ulimwenguni kote FIFA limeifungia timu ya taifa ya Iraq kucheza michezo yake katika uwanja wa nyumbani kwa sababu za kiusalama.

Taarifa iliyothitishwa na uongozi wa chama cha soka nchini Iraq imeeleza kwamba FIFA wameazimia kuifungia timu hiyo kucheza katika uwanja wake wa nyumbani kutokana na msongamano wa mashabiki ulionekana katika mchezo wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 dhidi ya Jordan ambapo wenyeji walikubali kisago cha mabao mawili kwa moja.

Raisi wa chama cha soka nchini Iraq Najih Hmoud amesema wameipokea taarifa hiyo kwa masikitiko makubwa na katu hawawezi kupinga maamuzi yaliyotolewa dhidi yao zaidi ya kuushauri uongozi wa shirikisho la soka Ulimwenguni FIFA kufikiria upya maamuzi waliyoyatoa.

Amesema uwanja wa Franso Hariri uliopo katika mji wa Arbil ambao hutumiwa kama uwanja wa nyumbani wa timu ya taifa ya Iraq upo katika hali ya usalama na kiujumla mji husika upo katika hali ya kuridhisha mbali na miji mingine ambayo inahofiwa kuwa na fujo.

Mbali na timu ya taifa ya Iraq kufungiwa kucheza michezo wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 katika ukanda wa barani Asia, pia timu hiyo imefungiwa kutoutumia uwanja huo katika michezo ya kuwania nafasi ya kucheza michezo ya Olympic ya mwaka 2012.


Kwa mantiki hiyo sasa michezo nyumbani itakayohusishwa timu ya taifa ya Iraq, itakuwa ikichezwa nje ya nchi hiyo.

Timu ya taifa ya Iraq ambayo ipo katika nafasi ya 109 katika viwango vya ubora wa soka duniani inakamata nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi la kwanza ambalo linazijumuisha nchi za Jordan, China pamoja na Singapore na hii ni kwa upande wa kuwania kinyang’anyiro cha kucheza fainali za kombe la dunia za mwaka 2014.

No comments:

Post a Comment