KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, September 22, 2011

Owen Hargreaves AREJEA UWANJANI KWA MAKEKE.

Juhuzi zilizoonyeshwa na kiungo aliejiunga na Man City katika kipindi cha usajili kilichomalizika August 31 mwaka huu Owen Hargreaves katika mchezo wa kuwania kombe la ligi usiku wa kuamkia hii leo dhidi ya Birmingham City, zimemfanya Roberto Mancini kufanya utabiri wa kurejeshwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza.

Roberto Mancini amesema aliamua kumpa nafasi kiungo huyo katika mchezo huo kwa makusudi kwa lengo la kuwaonyesha mashabiki wa soka ulimwenguini kote ni vipi Owen Hargreaves, alivyorejea katika ulimwengu wa soka baada ya kukaa nje kwa muda mrefu kutokana na sababu za kuwa majeruhi.

Amesema juhuzi binafsi pamoja na zile za ushirikiano wa kikosi cha Man city zitamfanya Owen Hargreaves, kurejeshwa katika timu ya taifa ya Uingereza, endapo mambo yatamuendea vizuri msimu huu, huku akiomba balaa la majeruhi limkalie mbali.

Owen Hargreaves alifunga bao la kwanza katika dakika ya 17 na bao la pili likapachikw akimiani na Super Mario Balotelli katika dakika ya 38.
Hata hivyo Owen Hargreaves alitolewa katika dakika ya 57 na nafasi yake kuchukuliwa na James Milner.

Amesema ni faraja kubwa sana kwake kurejea tena uwanjani na ulikua wakati mzuri wa kufanya vyema kutokana na ushauri aliokuwa akipewa na jopo la madaktari wa klabu ya Man City ambao toka alipojiunga klabuni hapo wamekua wakimfuatilia kwa umakini.

No comments:

Post a Comment