KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, September 22, 2011

Steven George Gerrard AREJEA UWANJANI BAADA YA MIEZI SITA.

Nahodha na kiungo wa klabu ya Liverpool Steven George Gerrard jana alirejea kwa mara ya kwanza uwanjani baada ya kusubiri kwa muda wa miezi sita iliyopita kutokana na majeraha.

Steven Gerrard alirejea uwanjani akitumika kama mchezaji wa akiba katika mchezo wa kuwania kombe la ligi dhidi ya Brighton and Hove Albion waliokua nyumbani huko Amex Stadium.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31 alichukua nafasi ya mshambuliaji kutoka nchini Uruguay Luis Alberto Suarez Diaz katika dakika ya 75.

Kurejea kwake uwanjani amekiri kumefurahisha kwani alisubiri kwa muda mrefu ambao amesema hatua hiyo imemsaidia kutazama mengi yaliyokua yakifanyika kikosini hivyo ameahidi kufanya makubwa kwa ushirikiano uliopo chini ya meneja wa Liverpool King Kenny Daglish.

Matokeo ya michezo mingine iliyochezwa usiku wa kuamkia hii leo katika michuano ya kiwania kombe la ligi ni pamoja na:


Cardiff City Stadium, Cardiff
Cardiff City 2 – 2 (7-6) Leicester City

St. Mary's Stadium, Southampton
Southampton 2 - 1 Preston North End

No comments:

Post a Comment