
Mkurugenzi wa ufundi wa PSG Leonardo Nascimento De Araujo amenukuliwa katika mtandao wa klabu hiyo akisema wanatazama uwezekano wa kutuma ofa ya kutaka kumsajili Carlos Tevez, kitakapofika kipindi cha usajili wa dirisha dogo mwezi januari mwakA 2012.
Amesema wanatambua kwa sasa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, ana matatizo makubwa ya uongozi wa Man City hivyo wanatumia nafasi hiyo kutaka kumaliza mzozo unaoendelea huko Etihad Stadium kwa muda wa juma moja sasa.

Mbali na klabu ya PSG, pia klabu inayochipukia kwa kasi kubwa huko nchini Urusi ya Anzhi Makhachkala inahusishwa na taarifa za kutaka kumsajili Carlos Tevez huku klabu yake ya zamani wa West Ham Utd ikiondolewa katika utaratibu huo baada ya viongozi wa Man City kutupilia mbali taarifa zilizotolewa na mmoja wa wamili wa klabu hiyo ya magharibi wa mji wa London.
No comments:
Post a Comment