KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, October 4, 2011

NIKIPEWA ARSENAL NIPO TAYARI - Carlo Michelangelo Ancellotti.

Aliekua meneja wa Chelsea Carlo Michelangelo Ancelotti amesema yupo tayari kukinoa kikosi cha Arsenal endapo uongozi wa klabu hiyo utaamua kuachana na meneja wa sasa Arsene Wenger endapo watamkata awe nao huko Emirates Stadium.

Carlo Michelangelo Ancelloti ametoa msimamo huo huku akimini kabisa ipo siku atarejea katika ligi kuu ya soka nchini Uingereza baada ya kudumu kwa muda wa miaka miwili akiwa na klabu ya Chelsea ambayo aliipa ubingwa wa nchini Uingereza katika msimu wa mwaka 2009-10.

Meneja huyo mwenye umri wa miaka 52 amesema Arsenal ni klabu nzuri na wala hatosita endapo atatakiwa kuwa mkuu wa benchi la ufundi la klabu hiyo ambayo ametamba bado ina nafasi nzuri ya kufanya maajabu katika msimu huu wa ligi licha ya kuanza vibaya.

Amesema mbali na klabu ya Arsenal pia anatamani kuwa meneja wa klabu kubwa kama Tottenham Hotspurs ama Liverpool ambazo kwa sasa zimekaa katika mstari mzuri wa kupata ushidni kwenye michezo inayowakabili.

Wakati huo huo kipa namba moja wa klabu ya Arsenal Wojciech Szczesny, amakataa kata kata kukubaliana na madai ya baadhi ya mashabiki wa soka nchini Uingereza ambao wanadai kwamba Spurs kwa sasa ipo juu zaidi ya The Gunners ambao siku za nyuma walikua wakitamba katika upinzani wa klabu hizo mbili.

Kipa huyo amekataa kukubalia na madai hayo ya mashabiki kwa kusema kigezo cha kupoteza mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita hakiwezi kutumika katika uwiyano wa viwango kwa klabu hizo.

Amesema bado anaamini Arsenal wapo juu zaidi ya Spurs huku akitoa angalizo kwa mashabiki wanaowabeza kwa kuelza wazi kuwa, hiki ni kipindi cha mpito kwao kwani anaamini watarejea katika njia nzuri ya ushindi siku za hivi karibuni.

2 comments: