KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, October 4, 2011

Roman Abramovich APANIA KUIHAMISHA CHELSEA.

Mmiliki wa klabu ya Chelsea Roman Abramovich amedhamiria kubadilisha historia ya klabu hiyo baada ya miaka 106 kupitia, kwa kuhamisha makazi kutoka Stamford Bridge hadi katika eneo lingine huko mjini London nchini Uingereza.

Roman Abramovich alikua na matarajio ya kuuendeleza uwanja wa Stamforde Bridge kwa kuubomoa na kuutengeneza upya lakini utaratibu huo umepiga hatua na kufikiria kununua sehemu nyingine kwa ajili ya kujenga uwanja mpya ambao utakua chachu ya kupata makazi mapya ya klabu hiyo.

Tayari kibopa huyo ameshanunua sehemu ambayo ni karibu wa uwanja wa sasa, na endapo dhana ya kujenga uwanja mpya itakamilika basi Chelsea wataingai kati utaratibu wa kuwa miongoni mwa vilabu vitakavyomiliki uwanja utakaokuwa na uwezo wa kuchukua mashabiki elfu 60.

Hata hivyo ifahamike kwamba kwa sasa Roman Abramovich hana sauti ya umiliki wa uwanja wa Stamford Bridge, zaidi ya kuomba namna ya kununua hisa kutoka kwa mashabiki wa Chelsea wenye haki ya umiliki baada ya kufanya maboresho miaka 14 iliyopita.

Kutokana na hali hiyo Roman Abramovich ametoa offer ya paundi milioni 10 ili kulipa fidia ya hisa za mashabiki na pia yu tayari kulipa sehemu ya mkopo wanaodaiwa mashabiki hao wa paundi milioni 8.5 ambao ulitumika wakati wa kufanyika kwa marekebisho ya uwanja wa Stamforde Bridge.

Kwa upande wa mwenyekiti wa klabu hiyo Bruce Buck amesema ana imani wanahisa wa Chelsea watakubaliana na andiko hilo la Roman Abramovich.

BONGE LA BIFU NDANI YA FULHAM.

Meneja wa klabu ya Fulham Martin Jol ameingia katika vita kali na baadhi ya wachezaji wake baada ya kuwatoza faini ya paund 500, kufuatia kitendo cha kukosa penati katika mchezo wa mzunguuko wa tatu wa kombe la ligi *Curling Cup* dhidi ya Chelsea mnamo September 21.

Martin Jol ameamua kufanya hivyo akichulia kama sehemu ya kuwafunda wachezaji wake ili waweze kutambua umuhimu wa kusaka ushindi pale inapohitajika na si kufanya vitendo vya kizembe na kuigharimu klabu inayowategemea kwa kiasi kikubwa.


Mmoja wa maafisa wa klabu ya Fulham amesema kitendo hicho kimewakera mno wachezaji waliokatwa pesa hizo, hatua ambayo inaendeleza upinzani miongoni mwao dhidi ya Martin Jol alietangazwa kuchukua nafasi ya Mark Hughes miezi miwili iliyopita.

Orlando Sa mshambuliaji kutoka nchini Ureno alikosa mkwaju wa penati katika muda wa kawaida baada ya kuangushwa katika eneo la hatari, hatua ambayo iliinyima nafasi Fulham kusonga mbele kupitia muda wa kawaida.

Nae Pajtim Kasami kiungo kutoka nchini Macedonia alikosa mkwaju muhimu wa penati baada ya timu hizo kwenda sare ya bila kufungana katika muda wa dakika 120, hatua ambayo ilitoa mwanya kwa Chelsea kuendelea katika michuano ya kombe la ligi.

Itakumbukwa kwamba penati ya Kasami iligonga mwamba na kuifanya Chelsea kupata ushindi wa peneati 4-3.

NIKIPEWA ARSENAL NIPO TAYARI - Carlo Michelangelo Ancellotti.

Aliekua meneja wa Chelsea Carlo Michelangelo Ancelotti amesema yupo tayari kukinoa kikosi cha Arsenal endapo uongozi wa klabu hiyo utaamua kuachana na meneja wa sasa Arsene Wenger endapo watamkata awe nao huko Emirates Stadium.

Carlo Michelangelo Ancelloti ametoa msimamo huo huku akimini kabisa ipo siku atarejea katika ligi kuu ya soka nchini Uingereza baada ya kudumu kwa muda wa miaka miwili akiwa na klabu ya Chelsea ambayo aliipa ubingwa wa nchini Uingereza katika msimu wa mwaka 2009-10.

Meneja huyo mwenye umri wa miaka 52 amesema Arsenal ni klabu nzuri na wala hatosita endapo atatakiwa kuwa mkuu wa benchi la ufundi la klabu hiyo ambayo ametamba bado ina nafasi nzuri ya kufanya maajabu katika msimu huu wa ligi licha ya kuanza vibaya.

Amesema mbali na klabu ya Arsenal pia anatamani kuwa meneja wa klabu kubwa kama Tottenham Hotspurs ama Liverpool ambazo kwa sasa zimekaa katika mstari mzuri wa kupata ushidni kwenye michezo inayowakabili.

Wakati huo huo kipa namba moja wa klabu ya Arsenal Wojciech Szczesny, amakataa kata kata kukubaliana na madai ya baadhi ya mashabiki wa soka nchini Uingereza ambao wanadai kwamba Spurs kwa sasa ipo juu zaidi ya The Gunners ambao siku za nyuma walikua wakitamba katika upinzani wa klabu hizo mbili.

Kipa huyo amekataa kukubalia na madai hayo ya mashabiki kwa kusema kigezo cha kupoteza mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita hakiwezi kutumika katika uwiyano wa viwango kwa klabu hizo.

Amesema bado anaamini Arsenal wapo juu zaidi ya Spurs huku akitoa angalizo kwa mashabiki wanaowabeza kwa kuelza wazi kuwa, hiki ni kipindi cha mpito kwao kwani anaamini watarejea katika njia nzuri ya ushindi siku za hivi karibuni.

PSG WAJIPANGA KUMSAJILI TEVEZ.

Ikiwa imepita siku moja baada ya kufanya mazungumzo na uongozi wa klabu ya Man City, mshambuliaji kutoka nchini Argentina Carlos Tevez, anahUsishwa na taarifa za kuwa mbini kuondoka klabuni hapo na kusajiliwa na vibopa wa ligi ya nchini Ufaransa Paris Saint-Germain.

Mkurugenzi wa ufundi wa PSG Leonardo Nascimento De Araujo amenukuliwa katika mtandao wa klabu hiyo akisema wanatazama uwezekano wa kutuma ofa ya kutaka kumsajili Carlos Tevez, kitakapofika kipindi cha usajili wa dirisha dogo mwezi januari mwakA 2012.

Amesema wanatambua kwa sasa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, ana matatizo makubwa ya uongozi wa Man City hivyo wanatumia nafasi hiyo kutaka kumaliza mzozo unaoendelea huko Etihad Stadium kwa muda wa juma moja sasa.

Amesema kwamba Carlos Tevez, bado ana uwezo mkubwa wa kucheza soka na anaamini atakapobadilisha mazingira, atakuwa na uhuru wa kufanya makubwa zaidi hivyo wanasubiri na kutazama uwezekano wa kumsajili mwezi januari endapo mipango yao itakwenda kama wanavyotarajia.

Mbali na klabu ya PSG, pia klabu inayochipukia kwa kasi kubwa huko nchini Urusi ya Anzhi Makhachkala inahusishwa na taarifa za kutaka kumsajili Carlos Tevez huku klabu yake ya zamani wa West Ham Utd ikiondolewa katika utaratibu huo baada ya viongozi wa Man City kutupilia mbali taarifa zilizotolewa na mmoja wa wamili wa klabu hiyo ya magharibi wa mji wa London.

Monday, October 3, 2011

Hamburg SV WAPO MSTUNI WAKISAKA MENEJA MPYA.

Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Hamburg SV Frank Arnesen amesema klabu hiyo itakua chini ya meneja mpya mara baada ya kumalizika kwa wiki ya michezo ya kimataifa iliyoanza hii leo.

Frank Arnesen ametoa angalizo hilo, baada ya kikosi cha klabu hiyo inachoshiriki ligi kuu ya soka nchini Ujerumani, kuwa chini ya meneja wa muda Rodolfo Cardoso ambae amekua akiifanya kazi hiyo bila ya kuwa na sifa zinazohitajiwa na shirikisho la soka barani ulaya UEFA.

Rodolfo Cardoso ameifanya kazi hiyo kwa muda wa mwezi mmoja, na hii ilikuja baada ya kuondoka kwa meneja Michael Oenning alishindwa kutimiza malengo ya klabu.

Hata hivyo uongozi wa Hamburg SV ulikuwa umeshajipanga kufanya amzungumzo na Huub Stevens kwa ajili ya kumaliza tatizo la meneja klabuni hapo, lakini mpango huo ulikwenda tofauti baada ya kuwahiwa na viongozi wa Schalke 04 juma lililopita.

Lakini pamoja na mipango hiyo kuvurugika yasemekana uongozi wa Hamburg SV unajipanga kuzungumza na mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Sergei Barbarez ambae ameonyesha nia ya kuwa tayari kuyavaa majukumu ya umeneja huko Imtech Arena.

Francesco Totti KUREJEA UWANJANI KATI KATI YA OKTOBA.

Nahodha na mshambuliaji wa Associazione Sportiva Roma Francesco Totti anapewa nafasi kubwa ya kucheza mchezo ujao wa ligi kuu ya soka nchini humo ambao utawakutanisha na mahasimu wao wakubwa wa mjini Roma SocietĂ  Sportiva Lazio mnamo October 16.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 35, aliumia misuli ya paja mwishoni mwa juma lililopita ambapo AR Roma walikua na kibarua cha kuwakabili Atalanta ambao walikubali kichapio cha mabao matatu kwa moja.

Francesco Totti anapewa nafasi ya kurejea uwanjani baada ya majuma mawili kupita, huku mashabiki wa SS Lazio wakimkumbuka kwa mabao yake mawili yaliyowazamisha katika mchezo wa ligi msimu uliopita uliochezwa mwezi wa tatu.

Totti hii leo amefanyia vipimo na jopo la mdaktari klabuni hapo na imethibitika hakuumia sana na sasa anatarajia kuanza mazoezi mepesi siku chache zijazo tayari kwa mchezo huo.

AS Roma pamoja na SS Lazio ambao wote kwa pamoja wanautumia uwanja wa Olympico kama uwanja wao wa nyumbani, wapo sawa katika msimamo wa ligi ya nchini Italia baada ya kufikisha point 8 lakini The Giallorossi *AS Roma* wapo katika nafasi ya sita kwa kuwa na tofauti nzuri ya mabao ya kufungwa na kufunga.

BAKARI NJE MIEZI MITATU !!!

Beki wa pembeni wa klabu ya Arsenal Bacary Sagna, itamchukua muda wa miezi miwili hadi mitatu kurejea tena uwanjani baada ya kuumia akiwa katika mchezo wa jana wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza dhidi ya Tottenham Hotspurs walioibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja.

Daktari wa timu ya taifa ya Ufaransa Fabrice Bryand amethibitisha taarifa hizo kwa kusema kwamba Bacary Sagna hatokuwepo katika mchezo wa mwishoni mwa juma hili, ambapo mabingwa hao wa dunia wa mwaka 1998, watacheza mchezo wa kuwania nafasi kucheza fainali za mataifa ya barani Ulaya dhidi ya Albania.

Daktari huyo ametoa taarifa hizo kwa kushirikiana na jopo la madaktari wa klabu ya Arsenal ambao pia wamethibitisha kwamba beki huyo mwenye umri wa miaka 28 amevunjia mfupa wa mguu uitwao Fibula.

Tayari kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ufaransa Laurent Blanc ameshamuita kikosini beki wa pembeni wa klabu Lille Mathieu Debuchy kama mbadala wa Bakari Sagna kwa ajili ya kuendelea na kampeni ya kusaka tiketi ya kucheza fainali za mataifa ya barani Ulaya.

Bakari Sagna aliumia mguu baada ya kusukumwa na beki wa pembeni wa Tottenham hotspurs Benoit Assou-Ekotto hatua ambayo ilimfanya kuangukia mbao za matangazo pembezoni mwa sehemu ya kuchezea ya uwanja wa White Hart Lane.

Wakati huo huo viongozi wa klabu ya Arsenal pamoja na Spurs wamelaani vitendo vya ubaguzi wa rangi vilivyojitokeza katika mchezo wa jana pale klabu hizo zilipokutana huko kaskazini mwa jiji la London.

Viongozi wa pande hizo mbili wamesema daima wataendelea kushirikiana kwa kila hali na katu hawatochukizana eti kwa sababu ya mashabiki ambao walionyesha vitendo ambavyo vilikosa uungwana.

Kwa mujibu wa taariffa iliyotolewa kwa pamoja na pande hizo mbili inadai kwamba lugha za matusi, kejili pamoja na ubaguzi wa rangi zilitawala kwa mashabiki wa Arsenal pamoja na wale wa Spurs.

Kwa upande wa Arsenal walimkejeli mshambuliaji wao wa zamani Emmanuel Adebayor kwa kumzomea na kumuimbia nyimbo za kumkashifu kutokana na janga lililoikuta timu ya taifa ya Togo ilipokua ikielekea nchini Angola katika fainali za mataifa ya barani Afrika mwaka 2010.

Nao mashabiki wa Spurs waliwakashifu wachezaji wa Arsenal Alex Song pamoja na Bakari Sagna kwa kigezo cha rangi.

UONGOZI WA MAN CITY KUKUTANA NA TEVEZ.

Mshambuliaji kutoka nchini Argentina Carlos Tevez hii leo alitarajia kukutana na viongozi wa klabu ya Man city ikiwa ni sehemu ya kuendelea kwa uchunguzi unaofanya kufuatia tukio la kugoma kuingia uwanjani katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Fc Bayern Munich kati kati ya juma lililopita.

Tevez anakutana na uongozi wa klabu hiyo ya Etihad Stadium, huku akiwa anatumikia adhabu ya kufungiwa majuma mawili kufuatia tukio hilo ambalo lilipokelewa vibaya na wadau wa soka nchini Uingereza pamoja na huko nchini Ujerumani.

Sababu kubwa ya mkutano huo ni kutaka kufahamu upende wa Carlos Tevez ambao una haki ya kutetea kwa kile alichokifanya ambapo anadai hakukataa kuingia uwanjani kama ilivyoelezwa na meneja wa man city Roberto Mancini.

Katika moja ya taarifa za mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, alizozitoa mara baada ya kikosi cha Man city kuwasili mjini Manchester kikitokea nchini Ujerumani, ilieleza kwamba alikataa kufanya mazoezi ya kupasha mwili baada ya kutakiwa na Roberto Mancini kufanya hivyo kwa kuwa tayari alikua ameshapasha wakati wa mapumziko.

Endapo uongozi wa Man city utamkuta Carlos Teves na hatia juu ya tukio hilo huenda ukavunja makataba wake na kumuamuru aondokea Etihad Stadium akiwa kama mchezaji huru.

CAPELLO AWATEMA MAGWIJI KIKOSINI.

Beki wa Man Utd Rio Ferdinand pamoja na kiungo wa Liverpool Steven Gerrard wameachwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza ambacho mwishoni mwa juma hili kitahitaji matokeo ya sare ya aina yoyote ili kupata tiketi ya kucheza fainali za mataifa ya barani ulaya za mwaka 2012 zitakazochezwa nchini Poland na Ukraine.

Kocha mkuu wa timu hiyo Fabio Capello mapema hii leo aliita kikosi chake ambacho kinawakosa wachezaji wenye uzoefu huku wengine wakitemwa kutokana na sababu za kushuka viwango ama kuwa majeruhi katika kipindi hiki.

Mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs Jermain Defoe pamoja na beki wa Man City Joleon Lescott wameachwa katika kikosi hicho licha ya kuonyesha jitihada za kujituma katika michezo ya ligi huku mshambuliaji wa Fulham Bobby Zamora pamoja na kipa wa Bursaspor Scott Carson wakijumuishwa katika kikosi cha wachezaji 24.

Mshambuliaji wa mabingwa wa soka nchini Uingereza Man Utd ambae kwa sasa yupo vizuri Danny Welbeck pamoja na mfungaji wa bao la pili la ushindi kwa Tottenham Hotspurs dhidi ya Arsenal Kyle Walker wamejumuishwa pia.

Kikosi kamili kilichoitwa na Fabio Capello kwa upande;

Makipa:
Scott Carson (Bursaspor), Joe Hart (Man City), David Stockdale (Ipswich).

Mabeki:
Leighton Baines (Everton), Gary Cahill (Bolton), Ashley Cole (Chelsea), Phil Jagielka (Everton), Phil Jones (Man Utd), Micah Richards (Man City), John Terry (Chelsea), Kyle Walker (Tottenham).

Viungo:
Gareth Barry (Man City), Stewart Downing (Liverpool), Adam Johnson (Man City), Frank Lampard (Chelsea), James Milner (Man City), Scott Parker (Tottenham), Theo Walcott (Arsenal), Ashley Young (Man Utd).

Wambuliaji:
Darren Bent (Aston Villa), Andy Carroll (Liverpool), Wayne Rooney (Man Utd), Danny Welbeck (Man Utd), pamoja na Bobby Zamora (Fulham)

Saturday, October 1, 2011

ARSENE AMKINGIA KIFUA ADEBAYOR.

Meneja wa washika bunduki wa Ashburton Grove, Arsenal Arsène Wenger amesema haamini kama mashabiki wa klabu hiyo bado wanakereka na tabia ya mshambuliaji kutoka nchini Togo Emmanuel Sheyi Adebayo ya kushangilia kwa kejeli mara baada ya kufunga bao katika mchezo wa ligi uliowakutanisha The Gunnes dhidi ya Man city mwaka 2009 huko Etihad Stadium.

Arsene Wenger amesema tayari mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25, ameshaomba radhi na kila mmoja klabuni hapo ameshamsamehe na katu hawawezi kulifikiria jambo hilo, na kuacha shughuli nyingine za kimaendeleo huko Emirates Stadium.

Wenger amezunguzia suala hilo, ikiwa imesalia siku moja kabla ya mpambano utakaowakutanisha mahasimu wa kaskazini wa jiji la London Arsenal dhidi ya Tottenham ambao kwa sasa wanamuhodhi Adebayor baada ya kumsajili kwa mkopo akitokea Man City.

VITA YA MANENO YA KUPAMBANA.

Meneja wa klabu ya Chelsea Andre Villas Boas amesema bado anakabiliwa na mazingira magumu ya kuzifahamu timu pinzani ikiwa ni mara yake ya kwanza kukutana nazo katika mchuano ya ligi kuu ya soka nchini uingereza.

Andre Villas Boas amezungumzia suala hili linalomkabili kwa sasa, kufuatia mchezo wa kesho dhidi ya Bolton Wanderers ambao atakutana nao kwa mara ya kwanza toka alipojiunga na The blues akitokea Fc Porto mapema mwezi wa saba.

Amesema ni vigumu kucheza na klabu usiyoifahamu vizuri, lakini akasema mipango aliyoikuta huko Stamford Bridge imekua ikimuongoza kuvifahamu vikosi vya wapinzani pale wanapokutana navyo.

Meneja huyo mwenye umri wa miaka 33, ameendelea kueleza kwamba mpambano wa kesho ambao utaunguruma huko Reebok Stadium utakua na sura tofauti kutokana na nafasi waliopo Bolton kwenye msimamo wa ligi ambapo watahitaji kujipapatua na kuondoka mkiani.

Pia amemzungumzia meneja wa Bolton Wanderers Owen Coyle ambae alipewa jukumu la kukonoa kikosi hicho mwaka 2010, kwa lengo la kuinusuru klabu hiyo iliyokua mkiani na kwa bahati nzuri alifanikiwa kufanya hivyo.

Nae meneja wa Bolton Wanderers Owen Coyle akazungumzo kwa upande wake ni vipi anavyomchukulia meneja wa Chelsea Andre Villas Boas ambae alipewa shughuli hiyo mara baada ya kutimuliwa kazi Carlo Michelangelo Ancheloti.

Amesema meneja huyo ni mzuri licha ya kuwa na umri mdogo na mara kadhaa amekua akifuatilia namna anavyokinoa kiklosi cha Chelsea ambacho anaamini kesho kitaonyesha upinzani mkubwa dhidi ya kikosi cha Bolton Wanderers.

URENO KUWAKOSA WACHEZAJI MUHIMU KIKOSINI.

Kikosi cha timu ya taifa ya Ureno, kitaelekea katika mchezo wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya barani Ulaya, dhidi ya timu ya taifa ya Iceland mwishoni mwa juma lijalo huku kikiwakosa wachezaji wawili wa klabu ya Real Madrid.

Kikosi cha Ureno kitawakosa Pepe pamoja na Fabio Coentrao ambao kwa sasa wanauguza majeraha ya misuli waliyoyapata wakiwa na klabu ya Real Madrid.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ureno Paulo Bento amethibitisha taarifa hizo kwa kusema ameumizwa sana na hatua hiyo lakini hana budi kukubaliana na ukweli uliopo na kutazama ni vipi atakavyoweza kuwakabili Iceland siku ya ijumaa.

Amesema anadhani kwa sasa ni wakati wa kumtumia beki wa FC Köln ya nchini Ujerumani Henrique Sereno, pamoja na beki wa Valencia Ricardo Costa ambao ana hakika wana uzoefu wa kutosha wa kucheza michuano ya kimataifa.

Maamuzi ya meneja huyo pia yameendelea kuheshimu adhabu aliyopewa beki Ricardo Carvalho ambae alisimamishwa na chama cha soka nchini Ureno, kwa muda wa mwaka mzima baada ya kutoroka kambini na kisha kushindwa kutoa sababu zilizopelekea kufanya hivyo.


Katika hatua nyingine Paulo Bento amemuita kikosini winga wa Sporting Clube de Portugal Ricardo Quaresma pamoja na mshambuliaji wa zamani wa Benfica ambae kwa sasa anaitumikia Sporting Clube de Braga Nuno Gomes.

Timu ya taifa ya ureno ipo katika mazingira mazuri ya kupata nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya barani Ulaya baada ya kufikisha point 13, ikiwa sawa na timu ya taifa ya Denmark pamoja na Norway.

Cesc Fabregas AUMIA MAZOEZINI.

Kiungo kutoka nchini Hispania na klabu bingwa nchini humo FC Barcelona Cesc Fabregas huenda ikamchukua muda wa majuma matatu kurejea tena uwanjani baada ya kuumia akiwa mazoezini mapema hii leo.

Kiungo huyo ambae alijiunga na FC Barcelona mwezi August akitokea Arsenal ya nchini Uingereza, anakabiliwa na maumivu ya nyama za paja ambapo hatua hiyo inamfanya ajiunga na wachezaji wengine ambao ni majeruhi klabuni hapo kama Andres Iniesta, Alexis Sanchez pamoja na Ibrahim Afellay.

Kuumia kwake kunaendelea kumuumiza kichwa meneja wa Fc Barcelona Josep Pep Guardiola Isala, ambae alitarajia kumtumia katika mpambano wa kesho ambapo Barca watasafiri hadi huko Estadio El MolinĂłn kupambana na wenyeji wao Sporting Gijon.

Cesc Fabregas , pia analazimika kuondolewa katika timu ya taifa ya Hispania baada ya kuitwa na kocha mkuu wa timu hiyo Vicente del Bosque kwa ajili ya mpambano wa mwishoni mwa juma lijalo wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya barani Ulaya dhidi ya jamuhuri ya Czech na kisha mchezo dhidi ya Scotland.

Mpaka sasa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23, tayari ameshafunga mabao manne toka alipojiunga na Fc Barcelona akitokea Arsenal, hatua ambayo inaonyesha tayari ameshazoea mazingira ya huko camp Nou.

Victor Anichebe ATAMANI MCHEZO WA MWISHO WA NIGERIA.

Mshambuliaji kutoka nchini Nigeria Victor Anichebe amesema kwa sasa si mwenye furaha kufuatia majeraha yanayomkabilia ambayo yatamkosesha mchezo wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya barani Afrika dhidi ya timu ya taifa ya Guinea mwishoni mwa juma lijalo.

mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 tayari ameshatemwa katika kikosi ambacho kilichoitwa na kocha mkuu Samson Siasia aliepania kuipelekea timu ya taifa ya Nigeria katika fainali hizo ambazo zitachezwa nchini Gabon pamoja na Equatorial Guinea.

Victor Anichebe amesema ni wakati mgumu sana kwake kwa hivi sasa kufikiria ni vipi alivyokua anahitajika katika kikosi cha Super Eagles ambacho kitatakiwa kupata ushindi katika mchezo huo dhidi ya Guinea ili kujihakikishia nafasi ya kuwa miongoni mwa mataifa 16 ya barani Afrika yatakayoshiriki hapo mwakani.

Anichebe alipatwa na maumivu ya nyonga katika mchezo dhidi ya Madagascar uliochezwa mwezi uliopita, ambapo katika mchezo huo alichezeshwa kama mshambuliaji pekee, baada ya kocha Samson Siasia kuamua kutumia mfumo wa 4-2-3-1.

Hata hivyo bado mshambuliaji huyo ataendelea kuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi miwili ijayo, kufuatia majibu ya vipimo alivyofanyiwa siku za hivi karibuni.

MAANDALIZI YA LIGI YA MABINGWA AFRIKA.

Beki kutoka nchini Ghana pamoja na klabu ya Esperance ya nchini Tunisia Harrison Afful amesema ushirikiano na umoja ndani ya kikosi cha klabu hiyo, anaimani utakua chachu katika muendelezo wa kusaka mafanikio kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika.

Harrison Afful amehimiza suala hilo la mshikamano na umoja huku akiutazama mchezo wa hapo kesho wa ligi ya mabingwa barani Afrika ambao utawakutanisha na Al Hilal ya nchini Sudan huko mjini Khartoum.

Beki huyo amesema kwa sasa kikosi chao kinaishikilia dhana hiyo na wanaamini itawasaidia kufanikisha suala la upatikananaji wa ushindi wakiwa katika uwanja wa ugenini.

Hata hivyo amekiri kwamba mpambano huo utakua mgumu kwa pande zote mbili lakini wao wameshajiandaa kukabiliana na hali yoyote watakayokutana nayo kutoka kwa Al Hilal ambao watakua na nguvu ya kushangiliwa na mashabiki wao wa nyumbani.

Amesema kwa muda wa juma zima wamekua na mazungumzo na uongozi wa benchi la ufundi kuhusiana na mpambano wa hapo kesho na suala kubwa linalosisitizwa ni ushirikiano na umoja.

Harrison Afful anatarajia kujumuishwa kikosini hiyo kesho baada ya kumaliza adhabu ya kuonyesha kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya mabingwa wa zamani wa barani Afrika Al-Ahly kutoka nchini ambao walilazimishwa sare wakiwa nyumbani.

Friday, September 30, 2011

King Kenny Dalglish AWAHUSIA MABEKI WAKE.

Meneja wa majogoo wa jiji Liverpool King Kenny Dalglish ameitaka safu ya ulinzi ya kikosi chake kufanya juhudui ambazo zitawawezesha kufanya kazi kwa pamoja kwa lengo la kutoruhusu kufungwa katika mchezo wa ligi dhidi ya Everton utakaochezwa kesho huko Goodson Park.

King Kenny Dalglish ametoa wito huo kufuatia wachezaji wake kufanya vyema katika mchezo uliopita ambapo walifanikiwa kuchomoza na ushindi dhidi ya Wolves waliokubali kisago cha mabao mawili kwa moja.

Amesema endapo safu yake ya ulinzi itakua makini kuna uhakika wa kufanya vizuri hiyo kesho ambapo kutakua na upinzani wa hali ya juu kutokana na upinzani wa klabu hizo pale zinapokutana.

Hata hivyo sababu kubwa iliyopelekea King Kenny Dalglish kuwahimiza wachezaji wake wananaocheza nafasi ya ulizni ni kutotaka kurejesha tofauti kubwa ya mabao ya kufungwa na kufunga ambapo kwa sasa msimamo wa ligi unaonyesha Liverpool katika kipingele hicho hana bao analodaiwa.

Everton wao wataingia katika uwanja wao wa nyumbani hiyo kesho huku wakiwa na kumbu kumbu ya kupoteza mchezo uliopita ambapo walikubali kisago cha mabao mawili kwa sifuri kutoka kwa Man City waliokua nyumbani huko Etihad Stadium.

SIKUSTAHILI KUFANYA VILE.

Siku mbili kabla ya mchezo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza ambao utawakutanisha mahasimu wa kaskazini mwa jiji hilo, Tottenham Hotspurs dhidi ya Arsenal, mshambuliaji aliesajiliwa kwa mkopo huko White Hart Lane akitokea Man City Emmanuel Sheyi Adebayor, ametamba kuifunga The Gunners katika mchezo huo.

Adebayor ametamba kuifunga Arsenal katika mpambano huo wa siku ya jumapili, huku akiringia utaratibu mzuri alioanza nao mara baada ya kusajiliwa klabuni hapo, ambapo alifanikiwa kufunga bao lake la kwanza akiwa na Spurs katika mchezo dhidi ya Wolves.

Mshambuliaji huyo kutoka nchini Togo, amesema anaamini mchezo huo utakua mgumu kutokana na historia ya vikosi vya klabu hizo vinapokuatana, lakini atajitahidi kadri awezavyo, kuhakikisha anafanya mipango ya kuwanyanyua mashabiki wa Tottenham ambao tayari wameshamkubali kufuatai kazi nzuri aliyoifanya.

Hata hivyo Adebayor amekiri alifanya makosa pale aliposhangilia mbele ya mashabiki wa Arsenal baada ya kufunga bao dhidi ya klabu hiyo ambayo ilimuuza Man City kwa ada ya uhamisho wa paund million 25.

Nae meneja wa Spurs Harry Redknapp amesema wanakwenda katika mchezo huo wa jumapili huku wakiamini Arsenal ni wazuri na wala hawatowadharau kutokana na misukosuko iliyowapata siku za hivi karibuni.

Amesema anatambua umuhimu wa mchezo huo, na katu hawezi kujidaia matokeo ya michezo ya ligi ya msimu uliopita ambapo Spurs waliibuka na point nne baada ya kupata ushindi emirates stadium na kulazimisha sare white hart lane.

Titus Bramble AFUNGIWA.

Uongozi wa klabu ya Sunderland umetangaza kumsimamisha kwa muda, beki wa klabu hiyo Titus Bramble ambae anakabiliwa na tuhuma za ubakaji pamoja na kukutwa na dawa za kulevya.

Uongozi wa klabu hiyo ya Stadium Of Light, umemsimamisha beki huyo mwenye umri wa miaka 30, kwa kipindi ambacho hakikuwekwa wazi lakini taarifa zingine zinadai kwamba huenda akarejea kikosini mara baada ya kukamilika kwa kesi inayomkabili.

Adhabu hiyo pia inahusisha harakati za kufanya mazoezi na kikosi cha klabu ya Sunderland ambacho mwishoni mwa juma hili kutaendelea na mkakati ya kusaka point tatu muhimu katika ligi kuu ya soka nchini Uingereza mara baada ya kukubali kisago cha mabao mawili kwa moja kutoka kwa Norwich city mwanzoni mwa juma hili.

Titus Bramble alikamatwa na jeshi la polisi nchini Uingereza siku mbili zilizopita, na kufanyiwa mahojiano na askari wa jeshi hilo, lakini jana aliachiwa kwa dhamana.

SAKATA LA CARLOS TEVEZ LAENDELEA KUSUMBUA UINGEREZA.



Meneja wa mabingwa wa soka nchini Uingereza Man Utd Sir Alex Ferguson amemuunga mkono meneja wa klabu pinzani ya Man city Roberto Mancini kufuatia msimamo wake wa kutomuhitaji mshambuliaji kutoka nchini Argentina Carlos Tevez.

Sir Alex Ferguson amesema msimamo wa meneja huyo kutoka nchini Italia unaonyesha ni vipi alivyo na maamuzi yenye nguvu ndani ya klabu ya Man City ambayo ana hakika haimtazami yoyote yule klabuni hapo kwa uwezo ama umaarufu alionao.

Amesema mchezaji siku zote anastahili kutii amri anayoamrishwa na mkuu wake wa kazi na yeye binafsi hakufurahishwa na kitendo alichokionyesha mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka, 27 ambae pia aliwahi kuwa chini yake huko Old Trafford.

Na aliekua kiungo wa klabu ya Man Utd, Paul Scholes amesema anamuonea huruma Carlos Tevez kutokana na tukio lililojitokeza katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya FC Bayern Munich uliochezwa usiku wa kuamkia siku ya jumatano.

Paul Scholes amesema anamuelewa vizuri Carlos Tevez na kikubwa alichonacho katika tabia ni kuhitaji kucheza kila mara na linapojitokeza jambo kinyume na hilo hukasirishwa na hatua hiyo.

Amesema yeye binafsi anakumbuka mwaka 2001, aliwahi kugoma kutii amri ya Sir Alex Ferguson ambae alimtaka kuingia uwanjani kama mchezaji wa akiba katika mchezo wa kuwania kombe la ligi na matokeo yake alitupwa benchi katika mchezo dhidi ya Liverpool.

Wakati huo huo mmoja wa viongozi wa klabu ya West Ham Utd iliyomsajili Carlos Tevez mwaka 2006 na kumpelekea nchini Uingereza kwa mara ya kwanza akitokea Sports Corinthians Paulista ya nchini Brazil, amesema yupo tayari kumrejesha mshambuliaji huyo Upton Park kwa mkopo.

Taarifa hiyo imetoka huko jijini London huku viongozi wa Man City wakiendelea kutafakari hatua za kumchukulia mshambuliaji huyo baada ya kumsimamisha kwa majuma mawili na pengine huenda adhabu hiyo ikaongezwa baada ya kufanyika kwa uchunguzi.

Hata hivyo kuna taarifa kwamba wabeba nyundo hao wa London wapo tayari kumlipa Carols Teves mshahara wa paundi 250,000 kwa juma kwa muda wa miezi mitatu, mshahara ambao anaupata kwa sasa huko Etihad Stadium.

Wakati hayo yakijiri mshambuliaji mwingine wa Manchester City Edin Dzeko amemuomba radhi Roberto Mancini kufuatia kitendo cha utovu wa nidhamu alichokionyesha baada ya kutolewa nje katika mchezo dhidi ya Fc Bayern Munich na nafasi yake kuchukuliwa na Nigel De Jong.

Edin Dzeko amesema hakudhamiria kufanya kitendo cha kutupa, Track Sout bali alifanya hivyo baada ya kushindwa kutimiza malengo ya kuisaidia klabu yake ambayo tayari ilikua nyuma kwa idadi ya mabao mawili kwa sifuri.

Thursday, September 29, 2011

MFANYABIASHARA WA KIMAREKANI AWA RAISI WA AS ROMA.

Mfanya biashara kutoka nchini Marekani Thomas DiBenedetto ametangazwa kuwa raisi wa klabu ya AS Roma baada ya kukamilisha mipango ya kununua asilimia 67 ya hisa za klabu hiyo mwezi mmoja uliopita.

Thomas DiBenedetto anakuwa raisi wa 22 wa klabu hiyo ya mjini Roma, na sasa anaichukua kutoka mikononi mwa familia ya Sensi ambayo imekuwa madarakani kwa muda wa miaka 18 iliyopita.

Hatua za kutangazwa kwa mfanyabiashara huyo zimethibitishwa muda mchache baada ya masuala la kisheria kukamilishwa na mwanasheria wa benki UniCredit Roberto Cappelli ambae alipitia mipango yote ya kisheria na kuona haina doa kwa Thomas DiBenedetto.

Utaratibu wa kuthibitishwa na mwanasheria wa benki UniCredit, umekuja kufuatia Thomas DiBenedetto, kufanya kazi na benki hiyo kwa kipindi kirefu hatua ambayo ilipelekea kufanya mpango wa kuinunua AS Roma kwa uaminifu uliopo dhidi ya benki hiyo.

Kwa mantiki hiyo sasa Thomas DiBenedetto anakuwa raisi wa kwanza wa klabu ya AS Roma ambae si raia wa nchini italia pamoja na kuwa mmiliki wa klabu ya michezo katika ardhi ya nchi hiyo.

ROBERTO MARTINEZ AIKATAA MIPANGO YA KUMSAJILI DIOUF.

Meneja wa Wigan Athletics, Roberto Martinez amekanusha taarifa za kuwa mbioni kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Senegal El-Hadji Diouf.

Roberto Martinez amekanusha taarifa hizo huku akikiri uwepo wa mshambuliaji huyo katika mazoezi ya kikosi chake ambacho kinashiriki michuano ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza na mwishoni mwa juma hili kitashuka dimbani kucheza na Aston Villa.

Amesema El-Hadji Diouf amekua akifanya mazoezi na wachezaji wake, na hatua hiyo ilianza toka alipotemwa na klabu ya Blackburn ambayo ilichoshwa na tabia zake za utovu wa nidhamua ambazo alikua akizionyesha mara kwa mara.

Amesema mbali na mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30, pia kipa kutoka nchini Ghana Richard Kingson, amekua akifanya mazoezi na kikosi chake mara baada ya kutemwa na klabu ya Blackpool, ambayo ilishuka daraja mwishoni mwa msimu uliopita.

Hata hivyo Roberto Martinez ametoa sababu za kuwapokea wachezaji hao wawili katika mazoezi ya kikosi chake ambapo amedai kwamba uwepo wao kikosini unatoa changamoto ya uzoefu kwa wachezaji wake ambao wanahitaji msaada mkubwa katika suala hilo.

Lakini licha ya kukanusha taarifa za kutaka kumsajili El-Hadji Diouf, Roberto Martinez bado anaendelea na mchakatio wa kutaka kufanya usajili wa mchezaji mmoja ama wawili ambao watajiunga na wengine klabuni hapo kwa lengo la kuongeza nguvu ambayo inaonekana kupungua, hatua ambayo imesababisha vipigo katika michezo ya ligi.

Wakati huo huo Roberto Martinez amezungumzia mchezo wa mwishoni mwa juma hili dhidi ya Aston villa ambapo amesema utakua mchezo muhimu kwa kila upande zaidi ya masuala ya kibinafsi ya kila mtu anaehusika na mchezo huo.

Martinez amezungumzi suala hilo baada ya kuulizwa anajisikia vipi kuelekea Villa Park baada ya kuikataa ofa ya kuwa meneja wa klabu ya Aston Villa mwishoni mwa msimu uliopita.

TEVEZ APIGWA STOP ETIHAD STADIUM.

Uongozi wa klabu ya Man City umemsimamisha kwa muda wa majuma mawili mshambuliaji kutoka nchini Argentina Carlos Tevez kufuatia utovu wa nidhamu aliouonyesha katika mchezo dhidi ya Fc Bayern Munich usiku wa kuamkia jana huko Allianze Arena.

Uongozi wa klabu hiyo ya Etihad Stadium umefikia maamuzi hayo baada ya kupoa taarifa kamili kutoka kwa meneja Roberto Mancini ambae alikiri kuchukizwa na tabia aliyoonyeshwa na mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27.

Taarifa iliyotolewa imeeleza kwamba kwa kipindi cha majuma mawili, uchunguzi utafanyika wa kubaini nini chanzo kilichopelekea Caros Tevez kugoma kuingia uwanjani kama mchezaji wa akiba wakati tayari Bayern Munich walikua wanaongoza mabao mawili kwa sifuri yaliyofungwa na Mario Gomes.

Taarifa hio imeongeza kwamba Carlos Tevez akiwa anaendelea na adhabu hiyo hatoruhusiwa kufanya shughuli yoyote klabuni hapo pamoja na kujumuika na wachezaji wenzake watakapokua mazoezini.

Hata hivyo Roberto Mancini ameshatoa msimamo wake wa kutokua tayari kushirikiana na mchezaji huyo mpaka hapo mkataba wake utakapofikia kikomo ama kuondoka kama mchezaji atakaeuzwa kwenye klabu nyingine itakayokua tayari kumsajili.

Kama itakumbukwa vyema Carlos Tevez alitoa kauli yake mara baada ya kurejea nchini Uingereza wakitokea nchini Ujerumania mbapo alisema kuwa benchi la ufundi lilimuelewa vibaya kufuatia maamuzi aliyoyafanya, lakini akaahidi atakuwa tayari kufanya chochote atakachoagizwa kukifanya klabuni hapo.

Frank Lampard AKIRI KUKASIRIKA.

Mfungaji wa bao la Chelsea katika mchezo wa kundi la tano la michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Valencia CF uliochezwa usiku wa kuamkia hii leo huko Stadio Mestella Frank Lampard amekiri hakufurahishwa na hatua ya kutolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na mshambuliaji kutoka nchini Ivory Coast Solomon Kalou.

Frank Lampard amesema alistahili kuendelea kubaki kikosini kwa ajili ya kuongeza purukushani za kusaidiana na wengine katika harakati za kusaka ushindi wakiwa ugenini lakini mwisho wa siku walijikuta wakilazimishwa sare ya bao moja kwa moja.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 33, amesema kwamba mchezo wa jana ulikua mzuri sana kwake kutokana na uchezaji mzuri wa kikosi cha Chelsea ulioonyeshwa uwanjani na alidhani angemaliza katika dakika zote 90.

Hata hivyo amedai kwamba anaheshimu maamuzi ya meneja Andre Villas Boas ambae ndie mwenye jukumu la kuamua nani acheze tena kwa wakati gani na mchezo gani katika msimu mzima wa soka.

Katika hatua nyingine meneja wa klabu ya Chelsea Andre Villas Boas ameonyesha kufurahishwa na mpango wake wa kumjumuisha kikosini Frank Lampard katika mchezo dhidi ya Valencia CF.

Andre Villas Boas amesema mashabiki wengi walikua wanambeza kiungo huyo kwa kisingizio cha kushikwa kwa kiwango chake ambapo anadhani hali hiyo ilitokana na kutompanga katika michezo kadhaa iliyopita.

Amesema hatua ya kufunga bao katika mpambano huo imekuwa nzuri kwake na pia imekuja kwa wakati muafaka baada ya kuwatahadharisha mashabiki wanaombeza Frank Lampard.

Alex Chamberlain AZUA GUMZO.





Bao lililofungwa katika dakika ya 8 na mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Uingereza na klabu ya Arsenal Alex Chamberlain, limemfanya mchezaji huyo kuweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo aliefunga kupitia michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Alex Chamberlain aweka rekodi hiyo na kuvunja rekodi iliyokua inashikiliwa na kiungo wa klabu ya arsenal Theo Walcot ambae mwaka 2007 alipata nafasi ya kufunga bao katika michuano hiyo akiwa na umri wa miaka 18 na siku 221.

Alex Chamberlain ambae kwa sasa ana umri wa miaka 18 na siku 44, amesema amefarijika na hatua hiyo ambayo anaamini imekuja kutokana na juhudi zake pamoja na ushirikiano na wachezaji wengine waliokuwepo kikosini hiyo jana.

Amesema mbali na suala hilo pia hana budi kuwashukuru wale wote waliomuwezesha kufikia mafanikio ya kucheza katika klabu kubwa inayotambulika ulimwenguni kote hatua ambayo imemfanya acheze katika michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya ambapo jana ulikua mchezo wake wa kwanza.

Alex Chamberlain 18 yrs 44days..Olympiacos ...2011.
Theo Walcot 18 yrs 221 days.. Slavia Prague ...2007.
Jack Wilshare 18 yrs 291 days.. Shakhtar Donetsk...2010.
Rooney 18 yrs 340 days..Fenerbahce..2004.
Bekham 19 yrs 219 days.

Nae meneja msazidi wa klabu ya Arsenal Pat Rice ambae jana alikua mkuu wa benchi la ufundi kufuatia bosi wake Arsene Wenger aliemaliza adhabu ya kufungiwa michezo miwili na UEFA amesema ni jambo zuri kwa mchezaji mwenye umri mdogo kama Alex Chamberlain kupata mafanikio hayo.

Amesema ni mara chache sana kwa wachezaji kama winga huyo kufunga kwenye michuano mikubwa kama ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, hivyo bado akaendelea kusisitiza jambo la kufarijika na muonekano wa kikosi alichokipanga hiyo jana dhidi ya mabingwa wa soka toka nchini Ugiriki, Olympiacos ambao walikubali kibano cha mabao mawili kwa moja.

Bao la pili la Arsenal lilifungwa na beki wa pembeni kutoka nchini Brazil Andre Santos aliesajiliwa mwanzoni mwa msimu huu akitokea katika klabu ya Fenabahce ya nchini Uturuki huku bao la kufutia machozi la olympiacos likifungwa na David Fuster.

AC MILAN NI KIBOKO ULAYA.

Stadio Giuseppe Meazza, Milan
AC Milan 2 - 0 Viktoria Plzen


Matokeo ya michezo mingine ya ligi ya mabingwa barani Ulaya iliyochezwa usiku huu ni pamoja na:

Petrovskiy, St. Petersburg
Zenit St. Petersburg 3 - 1 FC Porto

BayArena, Leverkusen
Bayer Leverkusen 2 - 0 Racing Genk

Mestalla, Valencia
Valencia CF 1 - 1 Chelsea

Stade VĂ©lodrome, Marseille
Olympique Marseille 3 - 0 Borussia Dortmund

Emirates Stadium, London
Arsenal 2 - 1 Olympiacos

Donbass Arena, Donetsk
Shakhtar Donetsk 1 - 1 APOEL Nicosia

Dynamo Stadium, Minsk
BATE Borisov 0 - 5 FC Barcelona