KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, July 22, 2009

NITAWALIPA FADHILA.

Kiungo wa kimataifa toka jamuhuri ya Czech TOMAS ROSICKY amesema umefika wakati wa kulipa fadhila kwa mashabiki wa klabu ya Arsenal ambao walimsubiri kwa muda wa miezi 18 aliyokuwa nje akiuguza majereha yake ya goti pamoja na nyonga.


Kiungo huyo mwenye umri wa miaka, 28, amesema mashabiki wa klabu ya Arsenal, ni kweli walikuwa na hamu ya kumuona akirejea tena uwanjani, huku wakiwa na machungu ya kukosa usaidizi wake katika kikosi cha The Gunners hivyo halitokuwa jambo la busara endapo atashindwa kuwatimizia waliyokuwa wakiyasubiri toka kwake.


Aidha TOMAS ROSICKY amezungumzia juu ya hatua ya klabu yake kuwa kwenye wakati mgumu wa kutwaa mataji kwa muda wa msimu kadhaa hivi sasa, ambapo amebainisha wazi kwamba hatua hiyo jibu lake litapatikana hivi karibuni na The Gunners ulimwenguni kote watafurahi kama ilivyo kwa mashabiki wa vilabu vingine.

Siku mbili zilizopita nahodha wa klabu ya Arsenal Francis Fabregas alizungumza na televisheni ya klabu hiyo na kueleza wazi juu ya kurejea kwa Rosicky.

Fabregas amesema anaamini kurejea kwa kiungo huyo kutasaidia kuleta nguvu ndani kikosi chao ambacho kinatarajia kufanya mabadiliko ya kiushindani msimu ujao.

Katika hatua nyingine beki wa kimataifa toka nchini Ubelgiji Thomas Vamalen ambae amesajili wa klabu hiyo akitokea Ajax Asterdam nae amezungumzia hatua ya kufurahishwa kwake na kujiunga na klabu hiyo.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 23 amesema ni bahati ilioje kwake kusajiliwa na klabu kubwa kama Arsenal hivyo ni jukumu kwake kuhakikisha anacheza soka ambalo litaiwezesha klabu hiyo kubadilika kimtazamo inapokuwa uwanjani na nje ya uwanja.

Hata hivyo beki huyo amezungumzia juu ya upinzani ambao upo katika kikosi cha kwanza kwa kusema kwamba anaifahamu fika hali hiyo na kutambua kuwa nafasi anayocheza ina wachezaji wengi na wenye uwezo hivyo ni jukumu lake kujituma ipasavyo.

NGOJA NGOJA YA ARSENE WENGER !!!!!!!!!


Klabu ya Olympic Lyon ya nchini Ufaransa imeingia kati taratibu za meneja wa klabu ya Arsenal Arsen Wenger za kutaka kumsajili mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Morocco na klabu ya Bordeaux Marouane Chamakh.


Olympic Lyon wametanmgaza hatua hiyo ambayo inadhihirisha kwamba wapo katika mawindo makali ya kutaka kumsajili chamakh.


Akitangaza taratibu za kuvutiwa na mshambuliaji huyo, raisi wa klabu ya Olympic Lyon, Jean-Michel Aulas amesema wamevuitiwa na uchezaji wa Chamakh ambae anapigiwa upatu wa kuziba pengo lililoachwa wazi na Karim Benzema alietimkia huko nchini Hispania katika klabu ya Real Madrid.


Amesema ana imani mshambuliji huyo hatokataa kujiunga nao kufuatia mazingira yaliopo sasa kuyazoea mbali na kutoka nje ya Ufaransa ambapo huko mazingira yatakuwa mageni kwake na itamchukuwa muda kuonyesha soka lake la kisawa sawa.


Ikumbukwe kuwa meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger alivieleza vyombo vya habari kwamba, Chamakh ni chaguo lake la kwanza katika harakati zake za kumsaka mrithi wa nafasi ya Emmanuel Adebayor aliejiunga na Man City mwishoni mwa juma lililopita.

Tuesday, July 21, 2009

Sulaiman Al Fahim AFANIKIWA.


Mfanyabiashara wa kimataifa toka Dubai Sulaiman Al Fahim amethibitishwa kuwa mwenyekiti mpya wa klabu ya Porthmouth ambayo ni miongoni mwa vilabu vitakavyoshiriki ligi kuu ya soka nchini Uingereza msimu ujao.

Al Fahim amethibitishwa kushikwa wadhifa huo baada ya kusikika kwa taarifa za fununu kwa muda wa majuma madhaa kwamba yu mbioni kuinunuwa klabu hiyo hali ambayo hii leo imetimia na kuwekwa hadharani kupitia vyombo vya habari.

Mfanyabiashara huyo amechukuwa madaraka ya kuwa boss wa klabu hiyo kutoka kwa Alexandre Gaydamak ambae alikuwa akiimiliki klabu hiyo kwa asilimi kubwa ya hisa hatua ambayo sasa inadhihirisha ni vipi klabu hiyo itaanza kuingia kwenye ushindani wa kisoka pamoja na kibiashara.

HUNTELAAR AKUBALI YAISHE.


Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Uholanzi na klabu ya Real Madrid Klaas-Jan Huntelaar amekubali kujiunga na klabu ya Stuttgart ya nchini Ujerumani.

Klabu ya Stuttgart imekamilisha utaratibu huo wa usajili wa mchezaji huyo kwa lengo la kuziba mwanya ulioachwa wazi na mshambuliaji wao wa kimataifa toka nchini ujerumani Mario Gomez ambae amejiunga na klabu ya Bayern Munich kwa ada ya uhamisho wa paund million 20.

Mshambuliaji huyo anaondoka huko St Bernabeu, baada ya kuwekwa kwenye orodha ya wachezaji ambao wanatakikana kuuzwa katika kipindi hiki cha usajili kufuatia hatua za kusajili kwa wachezaji wengine klabuni hapo.

Miongoni mwa wachezaji ambao wametoa changamoto kwa Huntelaar kuondoka Real Madrid ni pamoja na Kaka, Cristiano Ronaldo pamoja na Karim Benzema.

Kukubali huko kwa Klaas-Jan Huntelaar kunamaliza uvumi wa klabu za nchini Uingereza zilizokuwa zinamuhitaji kwa udi na uvumba ikiwemo klabu ya Arsenal pamoja na Manchester City ambayo hata hivyo mwishoni mwa juma lililopita ilifanikiwa kumnasa mshambuliaji Emmanuel Adebayor.

Klabu nyingine ya nchini Uingereza iliyokuwa ikimuhitaji Klaas-Jan Huntelaar ni Tottenham ambayo ilionekana kupania kukamilisha uhamisho wake lakini ilishindwa kufikia malengo hayo baada ya kuvunjika kwa mazungumzo yaliyokuwa yanaendelea kati yao na uongozi wa klabu ya Real Madrid.

Samir Nasri AVUNJIKA.


Kiungo wa kimataifa toka nchini Ufaransa na klabu hiyo ya Arsenal Samir Nasri atakuwa nje ya uwanja kwa muda kufuatia kuvunjika mguu alipokuwa mazoezini hii leo.


Nasri ambae ni mmoja wa wachezaji wa Arsenal walioweka kambi na huko nchini Austria kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza huenda akawa nje ya uwanja wa muda wa miezi miwili ama mitatu, kwa mujibu wa madaktari wa klabu hiyo.


Kufuatia gharka hiyo kiungo huyo natarajia kukosa sehemu ya mwanzo wa msimu wa ligi kuu pamoja na baadhi ya michezo ya timu yake ya taifa ya Ufaransa ambayo inawania nafasi ya kufuzu kucheza kombe la duniani mwaka 2010.

SAFARI YA ETO'O IMEWADIA.

Meneja wa klabu ya Barcelona Pep Guardiola, ameliorodhesha jina la mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Cameroon Samuel Eto'o katika orodha ya wachezaji atrakaowauza katika kipindi hiki cha usajili.
Pep Guardiola ameliorodhesha jina la mshambuliaji huyo, huku kukiwa na taarifa za kuwepo uwezekano wa Eto’o kuelekea Gueisepe Meaza yalipo makao makuu ya klabu ya Inter Milan ambayo ipo tayari kumtoa Zlatan Ibrahimavic kuelekea huko Nou Camp kama sehemu ya kubadiolishana.

Akizungumzia hatua hiyo Pep Guardiola amesema umewadia wakati wa mshambuliaji huyo kuondoka klabuni hapo na kuwapisha wachezaji wengine kuleta changamoto tofauti za kiushindani hususan katika safu ya ushambuliaji.

Amesema mashabiki wengi wa klabu ya Barcelona ulimwenguni kote anajua watamueleza tofauti huku wengine watamjadili kwa kueleza kuwa amefanya makosa ya kutarajia kumuuza mshambuliji huyo lakini akaendelea kusisitiza kwamba safu yake ya ushambuliaji inahitaji changamoto tofauti.

Pep Guardiola ambae ni meneja aliepata mafanikio makubwa katika kipindi cha msimu mmoja aliokuwepo huko Nou Camp ametanabai halitokuwa jambo la muhimu kutomshukuru Eto’o kwa msaada mkubwa alioutoa klabuni hapo katika michuano mbali mbali hususan ile ya ligi ya mabingwa barani ulaya na katu kwa hilo hawatomsahau.

Itakumbukwa kuwa majuma kadhaa yaliyopita mshambuliaji huyo alionyesha dalili za kutokuwa tayari kuondoka klabuni hapo licha ya klabu ya Manchester City kuonyesha nia zote za kumuhitaji, kwa kudai kwamba anahitaji asilimia ya fedha za usajili wake kama mkataba unavyoagiza.

Samule Eto’o alisajiliwa na klabu ya Barcelona mnamo mwaka 2004 akitokea katika klabu ya Real Mallorca kwa ada ya uhamisho wa paund million 16.

HUU NI MTAZAMO WAKE JAMANI.


Kipa namba moja wa kikosi cha klabu ya Arsenal Manuel Almunia amesema anaamini kikosi chao msimu ujao kitacheza kwa mtazamo mpya mbali na ilivyokuwa msimu uliopita.

Kipa huyo wa kimataifa toka nchini Hispania amesema wazo hilo linamuijia katika fikra zake kufuatia muonekano wa kikosi chao ambacho kimeongezewa nguvu na wachezaji waliokuwa majeruhi kwa muda mrefu ambao sasa wanaonekana kuwa fit na kucheza katika viwango vyao vya kawaida.

Almunia mwenye umri wa miaka 32 amewataja wachezaji hao kuwa ni Tomas Rosicky Eduardo huku akimtaja Andrey Arshavin kuwa ni mchezaji ambae hakuweza kuonyesha makali yake kufuatia ugeni aliokuwa nao wakati akisajiliwa klabu hapo mwezi januari mwaka huu.

Hata hivyo Almunia ameongeza kuwa mbali wachezaji hao wenye uzoefu, pia anaamini vijana chipukizi walipo kwenye kikosi chao, nao watakuwa wamejifunza mengi hali ambayo imeleta changamoto katika vichwa vyao na kuwajengea hatua ya kiushindani wanapokuwa mashindanoni.

Amesema katika mchezo wao wa kujipima ubavu uliounguruma mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya klabu ya Barnet na kumalizika kwa sare ya mabao mawili kwa mawili, wachezaji wa Arsenal walionyesha umahiri mkubwa na kucheza soka lenye tofauti hivyo hatua hiyo ni moja ya kuona ni vipi walivyobadilika.

Wakati huo huo meneja wa klabu ya Arsenal Arsène Wenger ameutangazia umma wa mashabiki wa klabu hiyo kwamba bado jicho lake laendelea kumuangaza mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Morocco na klabu ya Bordeaux ya nchini Ufaransa Marouane Chamakh.

Arsen Wenger ametangaza hatua hiyo hii leo alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari ambapo amebainisha wazi kwamba mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ndio chaguo lake la kwanza endapo atahitaji kufanya usajili katika kipindi hiki.

Amesema mshambuliaji huyo ana uwezo mkubwa wa kuziba mwanya ulioachwa wazi na mshambuliaji Emmanuel Adebayor ambae siku mbili zilizopita alikamilisha dili la kujiunga na klabu ya Manchester City.

Akionyesha ni vipi alivyo na hamu ya kuongeza mchezaji kwa sasa, wenger amesema ameona mapungufu katika safu ya ushambuliaji wakati kikosi chake kikicheza na klabu ya Barnet mwishoni mwa juma lililopita hivyo upo umuhimu mkubwa wa kufanya hima ya kusajili mshambuliaji ambae anaeweza kuziba nafasi hiyo.


Kauli hiyo ya Arsene Wenger inadhihirishayupo katika harakati za kutaka kumsajili mshambuliaji mwingine katika klabu hiyo na kuvunja kauli ambayo aliitoa mwishoni mwa juma lililopita katika vyombo vya habari kwa kusema kwamba haoni sababu ya kusajili mshambuliaji kwa wakati huu kutokana na kuwepo kwa jibu hilo ndani ya wachezaji waliosalia klabuni hapo.




Monday, July 20, 2009

JOHN TERRY AENDELEA KUKANYWA.


Kiungo wa kimataifa toka nchini Uingereza na klabu ya Chelsea Frank Lampard amesema anaamini rafiki yake wa karibu John Terry ataendelea kusalia Chelsea na kuzitupilia mbali taratibu za kujiunga na klabu ya Manchester City.

Lampard amesema nahodha huyo wa klabu ya Chelsea bado ana mapenzi ya dhati na klabu yake ya sasa hivyo itamuuwia vigumu kuianza safari ya kuondoka Stamford Bridge na kuelekea City Of Machester.

Amesema pamoja na kuwepo kwa kila aina ya mvuto ambao unatolewea na uongozi wa klabu ya ManCity bado anaamini Terry hatovutiwa na hali hiyo.
Lampard, ambae alikaribia kujiunga na klabu ya Inter Milan inayofundishwa na meneja wa zamani wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho msimu uliopita, ameongeza kuwa haoni sababu ya John Terry kuondoka kwenye klabu ya Chelsea ambayo ina mafanikio makubwa mbali na klabu inayomuhitaji kwa sasa.

Hivi karibuni klabu ya Man City iliripotiwa kuwa tayari kumlipa John Terry paund lakini mbili kama mashahara wake kwa juma, iwapo atakubalia kujiunga na klabu hiyo.

LIVERPOOL WACHEMSHA KWA RAPID VIENA.

Steffen Hofmann


Klabu ya Liverpool usiku wa kumakia leo ilishindwa kufurukuta mbele ya klabu ya Rapid Vienna ya nchini Austria baada ya kuchapwa bao moja kwa sifuri.

Mchezo huo ambao ni wa kirafiki na wenye lengo la kuizandaa klabu hizo na msimu mpya wa ligi wa mwaka 2009-10 ulishiudia Liverpool wakipachikwa bao hilo na mshambuliaji wa Rapid Vienna Steffen Hofmann katika dakika ya 57.

Katika kipindi cha kwanza Rapid walipata bao kupitia kwa Erwin Hoffer ambapo hata hivyo bao hilo lilikataliwa na mwamuzi kwa madai ya kuwa mchezaji huyo alikuwa ameotea kabla ya kuukwamisha mpira nyavuni.

Hata hivyo Liverpool ilikuwa imesheheni wachezaji wake mahiri kama Steven Gerrard, Jamie Carragher pamoja na Yossi Benayoun.

Gerrard pamoja na Carragher walicheza katika kipindi cha kwanza huku Benayoun pamoja na mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Uholanzi Dirk Kuyt wakicheza katika kipindi cha pili kufuatia mabadiliko yaliyofanywa na meneja wao Rafael Benitez.

Beki wa kimataifa toka nchini Uingereza Glen Johnson ambae amesajiliwa na klabu hiyo kwa ajili ya msimu mpya wa ligi hapo jana alipumzishwa kufuatia kuykabiliwa na maumivu ya kifundo cha mguu aliyoyapata kwenye mchezo wa kati kati ya juma lililopita dhidi ya St Gallen.

WIGAN YAENDELEA KUJIIMARISHA.


Klabu ya Wigan Athletic imekamilisha usajili mshambuliaji wa kimataifa toka Trinidad na Tobago, Jason Scotland kwa ada ya uhamisho wa paund million 2.

Jason Scotland amejiunga na klabu hiyo ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza akitokea katika klabu yake ya daraja la kwanza nchini humo ya Swansea.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30 amesaini mkataba na klabu yake hiyo mpya wa miaka miwili na amesema ana amini muda huo utamuwezesha kuisadia kwa hali na mali Wigan katika msimu mpya wa ligi kuu.

Jason Scotland ameongeza kuwa imekuwa kama ndoto kwake kujiunga na klabu hiyo na kucheza ligi kuu ambayo kila kukicha ilikuwa kama sehemu ya mawazo yake na alijitahidi sana kuisaidia klabu yake ya zamani ya Swansea ili nayo siku moja iweze kuchea ligi hiyo ikitokea ligi daraja la kwanza.

Msimu uliopita mshambuliaji huyo aliweza kuipachikiwa klabu yake ya Swansea mabao 24 na hatua hiyo yasemekana imekuwa chanzo cha benchi la ufundi la klabu yake ya sasa kuanza kumfuatilia mpka kufanikiwa kumsajili.


MSIMAMO WA HUYU MZEE BALAA !!!!!!


Meneja huyo wa kimataifa toka nchini ufaransa amebainisha wazi kuwa anafahamu kwa sasa kila shabiki wa klabu ya Arsenal kwa sasa atakuwa na hamu ya kutaka kufahamu ni mchezaji yupi atakaesajiliwa klabuni hapo lakini kwake haoni sababu ya kuliharakisha jambo hilo.


Wenger amesema ukikitazama kikosi chake kwa sasa kuna washambuliaji walio mahiri kama Van Persie, Arshavin, Walcott, Bendtner pamoja na Eduardo huku Thomas Rosicky akitarajiwa kuwepo katika kikosi cha kwanza msimu ujao baada ya kupona majereha yake na mwishoni mwa juma lililopita alirejea katika mchezo wa kujipima nguvu ambao ulimazika kwa sare ya mbao mawili kwa mawili dhdi ya klabu ya Barnet.

Hata hivyo amesema atakuwa tayari kutumia ada ya uhamisho wa Adebayor iwapo atampata mchezaji alie na umakini mkubwa na mwenye uwezo wa kuisadia Arsenal katika michuano kadha wa kadha msimu ujao.

Katika hatua nyingine Arsene Wenger ameendelea kuweka wazi mapenzi yake ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Morroco na klabu ya Bordeaux ya nchini ufaransa Morouane Chamakh kwa kueleza kwamba bado ni chaguo lake la kwanza iwapo atalazinika kufanya usajili katika kipindi hiki.


BADO MITEGO YAENDELEA KWA TERRY.


Meneja wa klabu ya Man City Mark Hughes ameendelea kusisitiza bado anaamini nahodha na beki wa klabu ya Chelsea John Terry ana mipango ya kutaka kuelekea huko Eastlands *City Of Manchester*.

Hughes ameendelea kutoa msisitizo huo huku akifahamu fika uongozi wa klabu ya Chelsea siku za hivi karibuni ulitoa kauli ya kutokuwa tayari kumuuza beki huyo ambae pia yumo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza.

Akizungumza kupitia mtandao wa klabu ya Man City Hughes amesema kusajiliwa kwa beki huyo bado kunawezekana ndani ya kikosi chake hivyo utaratibu wa kuendelea kuushawishi viongozi wa klabu ya Chelsea unaendelea.

Amesema mbali na kuwepo katika harakati hizo bado klabu yake itaendelea kuwawinda wachezaji ambao wana uwezo wa kucheza katika kikosi cha Man city.



Sunday, July 19, 2009

EDEBAYOR MAASAALAM!!!!!!!!!!!!!!!!




Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Togo Emmanuel Adebayor usiku wa kuamkia leo amekamilisha taratibu za kujiunga na klabu ya Man City.

Man City wamekamilisha usajili wa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kwa ada ya uhamisho wa paund milion 25 akitokea kaskazini mwa jiji la London yalipo makao makuu ya klabu ilitokuw ainammiliki ya Arsenal.

Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kukamilisha usajili huo, Emmanuel Adebayor amesema ameelekea City Of Manchester kwa lengo la kujitengenea historia mpya ya maisha yake ya soka pamoja kuiweka Man City katika hadhi ya kiushindani.

Adebayor amesema mara kadhaa amekuwa akitaka kujiwekea historia ya maisha yake katika mchezo huo ambapo pamoja na kufanya hivyo akiwa na vilabu vingine pamoja na timu yake ya taifa, bado anatamani kuendelea kufanya hivyo akiwa na klabu yake mpya ya Man City.

Nae meneja wa klabu ya Man City Mark Hughes amesema ana hakika kuwasili kwa Emmanuel Adebayor katika kikosi chake ni ishara tosha ya kuendelea kumaliza tatizo la ukame wa mabao uliokuwa unakisumbua kikosi chake hivyo ana imani mshambuliaji huyo atamaliza tatizo hilo.

Ikumbukwe kuwa Emmanuel Adebayor kabla ya kujiunga na klabu ya Arsenal mnamo mwaka 2006 alikuwa anaitumikia klabu ya AS Monaco ya nchini Ufaransa.

Kusajiliwa kwa Emmanuel Adebayor kunaifanya klabu ya Man City kuendelea kuwa na mchakato wa kutaka kuiimarisha safu yake ya usahambuliaji ambayo kwa sasa ina wachezaji kama Carlos Tevez, Roque Santa Cruz, Robinho, Craig Bellamy pamoja na Benjani Mwaruwari.

Usajili huyo wa wachezaji hao ambao tayari wameshawika wakia na vilabu vingine umepea nguvu na mmiliki wa Man City Sheikh Mansour bin Zayed al Nahyan ambae amepania kuleta mapinduzi ya soka nchini Uingereza na kubadilisha taswira ya mtazamo wa nafasi nne za juu za ligi hiyo ambao mara kadhaa umekuwa haubadiliki.

Katika kipindi hiki cha usajili Adebayor anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na klabu hiyo ambayo tayari imeshawapata akina, Santa Cruz Gareth Barry, pamoja na Carlos Teves.

Kikubwa mbacho hakitasahaulika kwa mashabiki wa klabu ya Arsenal dhidi ya mshambuliaji huyo ni ile hatua yake ya kupachika mabao 30 ndani ya michezo 48 aliyocheza katika masimu wa mwkaa 2007-08.

Saturday, July 18, 2009

Tomas Rosicky arejea uwanjani.


Mashabiki wa klabu ya Arsenal hii itakuwa ni habari njema kwenu kufuatia kiungo wenu wa kimataifa toka jamuhuri ya Czech Tomas Rosicky hii leo kurejea tena uwanjani baada ya kuwa majeruhi kwa muda wa mwaka mmoja na miezi kadhaa iliyopita.


Tomas Rosicky amerejea uwanjani katika mchezo wa kirafiki kati ya timu yake ya Arsenal dhidi ya FC Barnet.

Mchezo huo umemalizika kwa sare ya mabao mawili kwa mawili.


Hii itakuwa taarifa mbaya kwa mashabiki wa klabu ya Man city kufuatia timu yao kupooteza mchezo wa kirafiki uliopigwa huko nchini Afrika ya kusini dhidi ya timu ya Orlando Pirates.

Man city wamepoteza mchezo huo kwa kuchapwa mabao mawili kwa sifuri.



Kwa wale wa Man utd furaha ipo kwao baada ya timu yao kuchomoza na ushindi wa mabao matatu kwa mawili dhidi ya Malaysia XI.

BABU AWASHANGAZA WENGI !!!!!!!

Klabu ya Manchester United imethibitisha kukamilisha usajili wa mshambuliaji Mame Biram Diouf kutoka klabu ya Molde FK kutoka nchini Norway.

Baada ya kukamilisha usajili huo mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21 amekopeshwa papo hapo katika klabu yake hiyo ya zamani mpaka mwezi January mwakani .

Pengine usajili huo utawashangaza wengi baada ya hivi majuzi Sir Alex Ferguson kutangaza kwamba asingefanya usajili mwingine kwa ajili ya msimu ujao baada ya kuwasajili akina Michael Owen, Antonio Valencia na Gabriel Obertan.

Hata hivyo bosi huyo wa mashetani hao wekundu amesema iliwalazimu kuchukua hatua za haraka kumsajili mshambulaji huyo wa kimataifa toka nchini Senegal baada ya kuwepo taarifa za klabu kadhaa kuonyesha nia ya kutuma offer ya kumsajili .

Diouf amezivutia klabu kama Arsenal, Ajax na PSV ingawaje klabu ya Tottenham ilikuwa imeshatuma offer mapema kwa lengo la kumsajili.

Juma lililopita mshambuliaji huyo alifanikiwa kuifungia klabu yake hat trick na kuisaidia kupata ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Brann.

Mshambuliaji huyo amefanikiwa kufunga mabao 30 katika michezo 62 aliyoichezea klabu ya FK Molde tangu asajiliwe.

Ikumbukwe kuwa Manchester United pia walimsajili mshambuliaji wake wa zamani Ole Gunnar Solskjaer kutoka katika klabu hiyo mwaka 2007.


DAVID BECKHAM AMKANYA JOHN TERRY.


Kiungo wa kimataifa toka nchini Uingereza na klabu ya LA Galaxy DAVID BECKHAM amemuonya beki John Terry afikirie kwa makini kabla ya kufanya uamuzi wa kuihama klabu yake ya Chelsea.

Beckham anatambua maumivu ya kuihama klabu ambayo alikuwa akiishabikia na kuichezea kwa muda wa miaka 10 ya Man utd na kuchukuwa maamuzi ya kujiunga na klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 34 amekumbushia jinsi alivyokuwa na ndoto ya kutaka kuichezea klabu ya Manchester utd maisha yake yote ya soka lakini haikuwa dhamira yake kuondoka Old Trafold bali ilimlazimu kuchukua hatua hiyo.


Amesema kufuatia mapenzi aliyokuwa nayo dhidi ya Man utd ilifikia wakati alikuwa amashindwa kuitazama klabu hiyo kupitia runinga kufuatia hatua ya kuumizwa na kitendo cha kuondoka klabuni hapo.

Beckham amesema mchezo wa soka una maajabu yake na mambo hujitokeza na kuubadilisha kubadilika wakati wowote lakini hadhani kama John Terry ataihama Chelsea kutokana na umuhimu wake ndani ya klabu hiyo.

Becks amesema mamilioni ya klabu ya Manchester City hayataweza kumfanya Terry kuwa na furaha aliyokuwa nayo kwa sasa hivyo amempa ushauri wa kuendelea kuwa na nia ya kuichezea klabu yake yake ya chelsea.


Becks amesema kwa jinsi anavyomfahamu "JT' yaani John Terry alivyo na mapenzi na mchezo wa soka na sio pesa atafanya uamuzi ambao utakuwa na manufaa kwake.


Friday, July 17, 2009

SAMUEL ETO'O KUTOLEWA KAMA SADAKA.


Raisi wa klabu ya Inter Milan Massimo Moratti amethibitisha taarifa za yeye kuwepo katika mazungumzo na uongozi wa klabu ya Barcelona ya nchini Hispania ambayo inataka kumsajili mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic.


Raisi huyo wa Internazionale amesema mazungumzo hayo ni baina yake na raisi wa klabu ya Barcelona Joan Laporta ambae yupo tayari kutoa kiasi cha fedha pamoja na mshambuliaji wake Samuel Eto'o kwa lengo la kukamilisha safari nya Zlatan huko Nou Camp.

MILANGO IWAZI KWA ALBERTO AQUILANI.


Uongozi wa klabu ya As Roma umekubali kufungua milango ya kuwawezesha Liverpool kutuma ofa ya kumsajili Alberto Aquilani.


Aquilani amekuwa akiripotiwa kuwa mbioni kusajiliwa na klabu ya Liverpool lakini uongozi wa klabu yake ulikuwa ukikanusha taarifa hizo kwa kuuelezea umma kwamba mchezaji huyo kamwe hatouzwa.


Meneja wa klabu ya AS Roma Luciano Spalletti amesema kwa sasa hana lolote la kuzungumza juu ya kuondoka ama kubaki kwa Aquilani, lakini akasisitiza kwamba njia ni nyeupe kwa mchezaji huyo kufikiria kama ataendelea kusalia Stadio Olympico msimu ujao ama la.


Kwa upande wake mkurugenzi wa klabu ya AS Roma Bruno Conti amethibitisha kuwepo kwa taratibu za klabu ya Liverpool kutaka kutuma ofa ya kutaka kumsajili mchezaji huyo hali ambayo amekubaliana nayo kwa kusema endapo ofa hiyo itawafikia wataifanyia kazi.


Aquilani, mwenye umri wa miaka 25, bado ana mkataba wa kuichezea klabu ya AS Roma mpaka mwezi June mwaka 2013.




Thursday, July 16, 2009

AFADHALI !!!!!!!!!!!!


Wafanyakazi wa ujenzi wa viwanja vya soka vya nchini Afrika kusini ambavyo vitachezewa fainali za kombe mwaka 2010 wapo kwenye mlolongo wa makubaliano yatakayowawezesha kupata nyongeza ya mshahara kwa lengo la kumaliza mgomo ulidumu kwa muda wa juma moja.


Wafanyakazi hao ambao idadi yao ni elfu 70 wanaendelea na mlolongo huo huku taarifa zikieleza kuwa baadhi yao wameshaanza kufanya kazi hii leo.


Hapo jana, vyama vya Wafanyakazi na waajiri nchini Afrika kusini walikuwa wakikamilisha majadiliano ya kusaini makubaliano ya mikataba ambayo itawawezesha wafanyakazi wa ujenzi wa viwanja hivyo kulipwa asilimia ya mshahara waliyokuwa wanaihitaji.


Makubaliano yaliyopangwa kuhusiana na nyongeza hiyo bado hayajatangazwa rasmi, lakini inaaminika kuwa waajiri na wafanyakazi wamekubaliana nyongeza ya asilimia 12, ambapo awali wafanyakazi hao walikuwa wakitaka asilimia 13.


Wafanyakazi hao walianza mgomo July 8 mwaka huu kwa madai ya kutaka kuongezewa asilimia ya mshahara wao.


Mgomo huo ulisababisha wasiwasi kwa baadhi ya miji kutoweza kukamilisha muda uliowekwa na kukabidhi viwanja hivyo mwezi Desemba mwaka huu.

BADO TERRY SASA !!!!!!!!!!!!!!!!???????

MARK HUGHES amemuomba John Terry kuhakikisha anaipa mgongo klabu yake ya Chelsea kwa lengo la kuongeza hatua ya kufanya mapinduzi ndani ya klabu ya Manchester City.

Boss huyo wa Man City amesema umewadia wakati kwa beki huyo wa kimataifa toka nchini Uingereza mwenye umri wa miaka 28 kubadilisha muelekeo wake wa kucheza soka katika mazingira mapya.

Hughes amesema kutokana na uzoefu wa beki huyo ambae ameichezea klabu yake ya Chelsea kwa muda mrefu anatakiwa kukabiliana na changamoto nyingine ili aweze kuendelea kutimiza ndoto zake.

Amesema lengo lake si kumshawishi Terry kwa sababu ya fedha bali anataka mchezaji huyo kujenga hatua ya kukabiliana na changamoto ambazo zinaweza kubadilisha muelekeo wake katika mafanikio ya hii leo na hapo baadae.

Hughes aliewahi kuuona uwezo wa Terry alipokuwa anaichezea klabu ya Chelsea kati ya mwaka 1995 na 1998 amesema mchezaji huyo ana uwezo mkubwa wa kuwa kiongozi kwa maana ya unahodha.

Meneja huyo ameongeza kuwa anaamini hatua ya kusajiliwa kwa mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Argentina Carlos Tevez kutawahamasisha wachezaji wengine nyota ulimwengini kujiunga na klabu hiyo.

NJIA NYEUPE KWA ADEBAYOR.

Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Togo Emmanuel Adebayor amefanikiwa kupimwa afya yake na anataraji kujiunga na klabu ya Manchester City baada ya kibali cha kufanyika kazi ndani ya klabu hiyo kuhakikiwa.

Adebayor anatarajiwa kuelekea City Of Manchester akitokea kwenye klabu ya ya Arsenal aliyoichezea kwa muda wa miaka mitatu na nusu ambayo imekubalidi dili la paund milion 25 kama ada ya uhamisho wake.

Mbali na klabu ya Manchester City kuonekana kufanikiwa kumsajili mshambuliaji huyo alieifungia The Gunners mabao 16 msimu uliopita vile vile Adebayor alikuwa akihusishwa na taarifa za kutaka kusajiliwa na klabu za AC Milan na Chelsea.
Katika hatua nyingine meneja wa klabu ya Manchester City Mark Hughes amesema bado klabu hiyo itaendelea kuwasajili wachezaji nyota kwa ajili ya kukijenga kikosi chake msimu ujao.

Akiongea na waandishi wa habari kuthibitisha kumsajili aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Manchester Uinted Carlos Tevez, meneja huyo amesema bado klabu hiyo inahitaji wachezaji katika nafasi kadhaa kabla ya kuhitimisha lengo lake la usajili.

Manchester City ina lengo la kuwa miongoni mwa klabu zilizo na vikosi bora msimu ujao hatua ambayo imedhihirika kufuatia klabu hiyo kutumia kiasi kikubwa cha fedha katika usajili.

Iwapo klabu hiyo itakamilisha usajili wa Adebayor itakuwa imefanikiwa kuwasajili wachezaji kutoka klabu tatu kati ya sita zilizokuwa katika nafasi za juu msimu uliopita.


SAFARI YA PETER CROUCH YAENDELEA.


MENEJA wa klabu ya Sunderland Steve Bruce amethibitisha kuwa angependa kumsajili mshambuliaji Peter Crouch licha ya kukiri bado hawajaafikiana na klabu ya Portsmouth kuhusu gharama za usajili wake.


Awali Crouch alihusishwa na taarifa za kutaka kujiunga na klabu ya Fulham, lakini meneja Steve Bruce ameendelea na mikakati yake ya kuhakikisha anamsajili mshambuliaji huyo huku uongozi wa klabu yake ukifanya mazungumzo na uongozi wa klabu ya Portsmouth .


Wakala wa Crouch amethibitisha kuwa mchezaji wake aliyefanikiwa kupachika mabao 16 katika michezo 49 akiwa The Pompey msimu uliopita yu sokoni.

Wednesday, July 15, 2009

Stewart Downing anaswa!!!!!!


Klabu za MIDDLESBROUGH imekubali kumuuza winga wake wa kimataifa toka nchini Uingereza Stewart Downing kwa gharama ya paund million 12 ambazo zimetolewa kama ada ya uhamisho na klabu ya Aston Villa.


Makubaliano ya vilabu hivyo viwili yanamfanywa winga huyo mwenye umri wa miaka 24 kuondoka nyumbani kwao alipozaliwa na kutarajia kuanza maisha mapya huko Birmingham yalipo makao makuu ya klabu ya Aston Villa.


Hata hivyo kwa sasa Downing yu mbioni kurejea katika hali yake ya kawaida baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo katika mguu.

Sheyi Emmanuel Adebayor.



Mashabiki wa klabu ya Arsenal wataendelea kuongea kuhusu kuondoka kwake lakini katu hawatomsahau katika michezo hii Sheyi Emmanuel Adebayor.



1. Emmanuel Adebayor v Tottenham (Premier League, September 15, 2007)
2.
Emmanuel Adebayor v Villareal (Champions League, April 7, 2009)
3.
Emmanuel Adebayor v Newcastle (Premier League, December 5, 2007)
4.
Emmanuel Adebayor v West Ham (Premier League, January 1, 2008)
5.
Emmanuel Adebayor v Tottenham (Carling Cup, January 22, 2008)


Sulaiman Al Fahim AIWANIA THE POMPEY.


Mfanya biashara mwenye asili ya kiarabu Sulaiman Al Fahim anafanya mazungumzo na uongozi wa klabu ya Portsmouth kutaka kuinunua klabu hiyo.


Al Fahim anafanya mazunguzo hayo mmiliki wa the Pompey Sacha Gaydamak kupitia kwa msemaji wake Ivo Ilic Gabara ambaye amebanisha kuwa mazungumzo hayo yanataji kumalizika mwishoni mwa mwezi huu.


Gabara amesema kwa sasa mazungumzo hayo yamefikia pazuri lakini hakuwa tayari kuweka wazi kiasi cha fedha walichoafikiana.

PAUND MILION 300 ZA MAN CITY HUENDA ZIKAPUNGUWA.

Imeelezwa kuwa zaidi ya paundi million 300 zimetengwa na klabu ya MANCHESTER CITY kwa ajili ya usajili huenda zikapunguwa pale kikosi cha klabu hiyo kitakaporejea toka nchini Afrika Kusini mwishoni mwa wiki hii.

Hatua hiyo imeelezwa kufuatia klabu hiyo kutuma offer ya paundi milioni 25 kwenye klabu ya Arsenal kwa lengo la kumsajili mshambuliaji wao wa kimataifa toka nchini Toga Emmanuel Adeboyor .

Adeboyor anataraji kusaini mkataba wa miaka mitano utakaomwezesha kuwepo huko Cit of Manchester na kulipwa mshahara wa paundi laki moja na elfu thelathini kwa juma.


Man city wameelekeza nguvu zao usajili kwa Adebayor baada ya kukatishwa tamaa na hatua ya kumsajili mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Cameroon na klabu ya Barcelona Samuel Etoo.
Iwapo Man City watafanikiwa kumsajili mshambuliaji huyo watakuwa wametumia jumla ya paundi milioni sitini halia mbayo huenda ikapunguza kiasi cha fedha za kumsajili nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza na klabu ya Chelsea John Terry iwapo uongozi wa klabu hiyo utafanikiwa katika hatua hiyo.

Kiasi kingine cha fedha kilichotengwa na Man City ni paundi milioni 40 kwa ajili ya Terry ambapo wamaahidi kumlipa mshahara wa paundi laki 2 na nusu kwa juma.

Mwezi uliopita mmiliki wa klabu hiyo Sheikh Mansour aliahidi kuwa tayari kukijenga kikosi cha klabu huyo hukua kitegemea ushirikiano mkubwa toka kwa watendaji wenzake klabuni hapo.

Tayari klabu hiyo imeshakamilisha usajili wa mshambulaiji wa kimataifa toka nchini Paraguay alietokea kwenye klabu ya Blackburn Rovers Roque Santa Cruz ambae atakuwa nalipwa mshahara wa paund elfu 80 kwa juma, kiasi ambacho ni mara mbili zaidi ya kiasa alichokuwa analipwa na klabu yake ya zamani.
Mchezaji mwingine aliesajiliwa klabuni hapo ni Gareth Barry ambae atakuwa nalipwa mshahara wa paund elfu 90,000 kwa juma.

Tuesday, July 14, 2009

BECKHAM AFIKIRIA KUREJEA NYUMBANI.

Kiungo wa kimataifa toka nchini Uingereza DAVID BECKHAM amefungua milango kurejea nyumbani kwenye ligi kuu ya soka nchini Uingereza.

Beckham mwenye umri wa miaka 34 amekiri atarejea nyumbani na hatua hiyo itakuwa kama changamoto kwake ya kupata nafasi ya kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kitakachoshiriki fainali za kombe la duniani za mwaka 2010 zitakazofanyika nchini Afrika Kusini.

Kiungo huyo wa zamani wa klabu za Man Utd na Real Madrid ya Hispania amesema wakati anaondoka nyumbani kwao hakuwa na wazo ya kurejea kwa lengo la kucheza soka kutokana na mapenzi yake kuangukiwa kwenye klabu aliyoipenda ya Man Utd halia mbayo ilimuweka kwenye mazingira ya kutokuwa tayari kuvaa jezi za klabu nyingine na kucheza na Man Utd.


Hata hivyo kiungo huyo ameongeza kuwa angependa kurejea tena nchini Italia baada ya kuichezea kwa mkopo klabu ya AC Milan msimu uliopita.

Katika hatua nyingine mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Marekani anayecheza soka katika klabu ya LA Galaxy Landon Donovan usiku wa kiamkia leo alikaa na meneja wa wa klabu hiyo Bruce Arena kwa lengo la kumaliza mgogoro wake na Bechkam uliozuka miongoni mwa wachezaji hao.

Kikao hicho kilihusu sana kauli iliyotolewa na Donovan kwenye vyombo vya habari dhidi ya Beckham ambayo ilidai kuwa kiungo huyo hana moyo wa uzalendo wa kuichezea klabu ya LA Galaxy na hali hiyo ilidhihirishwa na yeye mwenyewe pale alipojiunga na klabu ya Ac Milan kwa mkopo.


Mazungumzo hayo yalimalizwa salama wa salamini na kushudia Donovan akikiri kuwa alikosea kutoia kauli hiyo, halia mbayo ilipokelewa kwa mikopno miwili na na Beckham ambaye alilichukulia suala hilo kiungwana.







TEVEZ HUYOOOOOO !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!



Klabu ya Manchester City imekubali kumsajili mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Argentina ambae pia alikuwa mtumishi kwenye vilabu vya West Ham Utd pamoja na Manchester United vyote vya nchini Uingereza Carlos Tevez.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 amesajiliwa na klabu hiyo kwa mkataba wa miaka mitano baada ya kupita kwenye vipimo vya afya usiku wa kuamkia leo.

Meneja wa klabu ya Man City boss Mark Hughes amesema hakika amefanikiwa kumnasa mchezaji alie kwenye kiwango cha juu cha kimataifa na ana imani Teves atakuwa suluhisho la kuisaidia klabu yake kwenye ushindani wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza.

Tevez, anatarajiwa kuonekana uwanjani akiwa amevaa jezi nambari 32 ambapo namba hiyo amekuwa akiitumia katika vilabu vya West Ham pamoja na Manchester United.

RAFA ASEMA TORRES HAONDOKI ANFIELD.

MENEJA wa klabu ya Liverpool Rafa Benitez amethibitisha kupokea offer kutoka katika vilabu mbalimbali zenye lengo la kutaka kumsajili mshambuliaji wa klabu hiyo toka nchini Hispania Fernando Torres.

Benitez amevitaja vilabu vilivyotuma offer zao huko Anfiled ni pamoja na Chelsea, Manchester City, Manchester United na klabu ya Real Madrid


Aidha amewataja viungo wake Xabi Alonso na Javier Mascherano pia wameemdelea kuwa kwenye mtiririko wa kutakiwa na baadhi ya vilabu barani ulaya .


Hata hivyo licha ya kupoke offer hizo Benitez amethibitisha kuwa msambuliaji Torres ndiye aliyeonyesha nia ya kuendelea kubaki Anfield kwa msimu ujao.


Benitez ametoa wito kwa baadhi ya vilabu na kutaka vifahamu kwamba klabu hiyo ina kikosi imara na lengo la klabu hiyo ni kutaka kukiimarisha kikosi hicho, hivyo hawana mpango wa kuwauza baadhi ya wachezaji wao walio bora .

MANUEL ALMUNIA AITAMANI THREE LION.

MLINDA mlango wa klabu ya Arsenal MANUEL ALMUNIA amesisitiza kwamba atafurahi kama ataitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza.

Almunia ametimiza vigezo vyote vya kuichezea timu hiyo ya taifa ua Uingereza kutokana na kuwa na nafasi ya kupata hati ya kusafiria ya Uingereza ambapo fursa hiyo imekuja baada ya kuichezea klabu ya Arsenal kwa muda wa miaka mitano.

Kipa huyo mwenye umri wa miaka 32 amesisitiza kuwa itakuwa vigumu kwake kuitwa katika timu ya taifa ya Hispania baada ya kuzaliwa na kukuliwa nchini Uingereza hivyo itakuwa ni heshima kwake kuvaa jezi zenye alama ya simba watatu kifuani akimaanisha timu ya taifa ya Uingereza.

Iwapo ataitwa katika kikosi hicho anataraji kukutana na upinzani mkubwa kutoka kwa makipa wenzake David James, Rob Green, Ben Foster, Scott Carson na Paul Robinson wanaotaka nafasi ya kuwemo kwenye kikosi kitakachoshiriki fainali za kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini iwapo Uingereza itafuzu.

CARLO ANCELOTTI AANZA KUUNGURUMA.


MENEJA wa klabu ya Chelsea CARLO ANCELOTTI anaamini yeye kama mmoja wa viungo bora aliyefanikiwa kutwaa medali katika michuano ya klabu bingwa barani ulaya atapewa heshima ya kutosha na wachezaji wa klabu yake mpya.

Angalizo hilo limekuja ili kuwataka wachezaji wake wajue aina ya uongozi atakaoutumia wakati anatekeleza wajibu wake na kuongeza kuwa anapenda kuwaona wachezaji wanakuwa na bidii mazoezini.

Ancelotti amesema wakati anachezaji soka hakuwa mchezaji mkimya bali alikuwa na bidii uwanjani na hakupenda kushindwa na mchezaji yoyote wa timu pinzani hivyo angependa wachezaji wa klabu hiyo wamuheshimu kama meneja wao.

Amesema atakuwa mwamuzi katika masuala ya kiufundi lakini pia atawaheshimu wachezaji wake atakaofanya nao kazi ili kujenga mahusiano mazuri.


Amesema lengo lake ni kuwa na wachezaji watakaokuwa na uweza kucheza vizuri kwa kipindi kirefu klabuni hapo.

Kuhusu utovu wa nidhamu ulioonyeshwa na mshambuliaji Didier Drogba aliyefungiwa kucheza michezo minne katika michuano ya kombe la mabingwa msimu ujao , Ancelotti amesema anafahamu hali aliyokuwa nayo mshambuliaji huyo jambo ambalo linaweza kumtokea mchezaji yoyote anaehisi kuonewa.

Wakati huohuo ancelotti anakabiliwa na kibarua kigumu cha kumshawishi nahodha wa klabu hiyo John Terry kuendelea kubaki Stamford Bridge baada ya kuwepo taarifa za kutaka kusajili na klabu ya Manchester City.


Mwishoni mwa juma lililopita wawakilishi wa Terry alikutana na mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich na kuzungumza hatma ya mchezaji huyo kuendelea kubaki Chelsea.
Katika hatua nyingine mlinda mlango wa klabu hiyo PETR CECH ameshauriwa na madkari kuendelea kuvaa kinga kichwani.

Chech amesema madaktari wameshauri kuendelea kuwa na kinga baada ya kukiri kwamba bado hajapona vizuri.
Itakumbukwa kwamba kipa huyo wa Chelsea alipata mpasuko katika fuvu lake mnamo mwaka 2006 alipokuwa kwenye purukushani za kudaka mpira mbele ya mshambuliaji wa klabu ya Reading Stephen Hunt aliemgonga na goti.